CCM kumekucha: Raila Odinga sasa amponza Magufuli!


Kama ni suala la urafiki angemtembelea nyumbani kwake na sio kwenye mkutano wa hadhara. Tusichanganye urafiki na dhamana tulizopewa.
 
Mwaliko binafsi,maoni yake binafsi hakuna tatizo hapa.

Makosa yapo, hiyo ni nchi ya watu na huyu ni waziri wa tanzania, ikitokea Odinga akashindwa uchaguzi mahusiano ya kenya na tanzania yatakuwaje? au ikitokea ameshinda ule upande wa wakaenya walioshindwa watawatazamaje watanzania waishio kenya? hii ni busara tu ya kawaida magufuli hakupaswa kupanda jukwaani! Membe inabidi asema kauli ya Magufuli siyo msimamo wa Tanzania dhidi ya uchaguzi huo wa kenya!
 
siasa chafu zimetuharibu na sasa hata visafi tunavifananisha na uchafu,ccm wameharibu sana bongo zetu.
 
it wasnt a public rally,it was ODM's national deligates meeting. Magufuri alialikwa kama rafiki,akaongea kama rafiki.koso lake liko wapi?
 
Nchi yetu ina majuha wengi sana. Si madokta wala darasa la saba woteeeee AMANZI GE NYANZA.
 

Mkuu Bagamoyo nimepata picha kutoka kwa rifiki yangu mwana ODM ili kunipa yaliyojiri na ameshangaa kuona story ya mh Magufuli imepamba moto mkiniruhusu nitatoa hizo picha ili muone alivyojiassociate na baadhi ya prominent figures!
 
Last edited by a moderator:
PhD Hapo juu umesema vema, jamaa nafikiri hakuwakilisha chama wala selikari so kama rafiki ana uhuru wake.
 
Last edited by a moderator:


Nimeona ni vema pia tukajadili kupitia hizi picha nilizozipata kwa mwanachama wa ODM ni rafiki yangu nilisoma naye pale Nairobi University of Nairobi miaka hiyooo!
 

Attachments

  • ODM 1.JPG
    1.1 MB · Views: 31
Ati nani? Magufuli, ameropoka tena! Takwimu? Au utekelezaji wa sera za chama tawala kinachoongozwa na dokta jakaya mrisho kikwete!
Huyo ndiye magufuli, kama hutaki unaacha.
Huku kwetu anaitwa KIKURUMKI.
 
Kama ni suala la urafiki angemtembelea nyumbani kwake na sio kwenye mkutano wa hadhara. Tusichanganye urafiki na dhamana tulizopewa.

Waziri mwandamizi ktk serikali ya JMT ambaye hajui dhamana kubwa aliyonayo,amelewa chakari madaraka!
 
Hili so jambo jipya kufanyika katika siasa za africa. Odinga mwenyewe alienda Zimbabwe kumfanyia kampeni Tsavangirai kipindi kile cha uchaguzi. Baada ya Tsavangirai kukosa uraisi hatujaona kama kiuna ugomvi baina ya nchi hizo, kwa nini udhani kutakuwa na ugomvi wowote kati ya TZ na Kenya kwa kauli ya Magufuri?

Hapo hakuna issue, hivi kumesikika lawama zozote kutoka Kenya au si tumeamua kulikuza tu?
 
Kumbukeni wiki kadhaa zilizopita Uhuru Kenyatta na Ruto walifika Ikulu ya DAR na kuteta na JK. Vyombo vya habari viliripoti kiduchu. Lakini binafsi naamini walikuwa wanatafuta support ya TZ. Sasa Raila aliona si vizuri kutumia JK ila yeye apitie kwa MAGUFULI pengine si kwa sababu ya urafiki tu lakini vilevile jamaa aliona pengine Dkt. Magufuli anaheshimika hapa TZ, hivyo, akienda KENYA anawezabadilisha upepo wa siasa. Wakati huo huo, DKt. Magufuli alipaswa kumpa msimamo wake kuwa anakwenda lakini inaweza kutoa picha tofauti kwa serikali mbili hizo, kwamba CCM inamtaka RAILA na si wengine, na hapa ndipo alipaswa kutumia busara na si umaarufu! Hata hivyo, hakuomba ruhusa toka kwa MKUU wake wa kazi? Alieleza anakwenda kufanya nini? Je, Wakenya watapata picha gani kwa JK na CCM yake? Hapo hamna urafiki.
 
Magufuli ni mtendaji mzuri lakini nyuma ya utendaji wake ni mtu mwenye kupenda sifa. Kupenda sifa huku kunamfanya awe mtu asiyependa kushindwa na mara nyingine huleta matata.

Naamini huo si msimamo wa MAGAMBA lakini watapaswa kuwajibika kwa hili kama walivyowajibika kwa Kauli za Magufuli alizoongea kwenye kampeni Igunga. Mimi niliona kwenye taarifa ya habari on the same day na sikuamini nayoyasikia lkn nikadunda moyo konde nikijilazimisha kuamini kuwa siasa za Kenya zinaruhusu.

Hii ndio shida ya viongozi wetu wasiojua maana ya wanachokisema mpaka waambiwe mahakamani wakati wanashtakiwa.
 
MAKENE, nimekubali hilo neo KIKURUMKI! Kweli alikurumka bila kukokotoa hesabu ili kuwezajua madhara ya kampeni hiyo. Tena katika masuala ya KIDIPLOMASIA ni hatari kwenda kufanya mambo kama hayo! RAILA akishindwa na hao walowaponda wakashika DOLA, uhusiano wa TZ na KENYA utakuwaje?
 
Shida nyingine ni kwamba haya MAGAMBA huwa hayajifunzi. Huyu Magufuli na wampe kazi ambazo ni technical na sio za kisiasa. Igunga pale kaongea concrete na beams, akaona haitoshi akaongezea columns na cross section. Watu wakashanglia na CCM ikashindwa uchaguzi lkn wakachukua jimbo. Hatma yake ndio ile sasa
 
Kwa hiyo tuseme Magufuli anaunga mkono vyama vya upinzani ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…