Wazo zuri. Pia kama kuna uwezekano picha za video zitasaidia saidi.Sasa hivi nimempigia simu kiongozi wa CDM katika kampeni huko Igunga na kumpa wazo hilo, na amesema ataliwakilisha kwa wenzake ili waone kama itafaa nao kutumia picha za wajawazito wanaodhalilishwa katika nchi yao yenye utajiri mkubwa.
taratibu kidogo...twende tartibu....
kwamba umesoma Mwananchi ndo ukaja na hizi hoja, au hii ni habari kwenye gazeti la Mwananchi?
anyhow, ulichokiandika kina mashiko kwa sababu kama sasa tunakwenda kwa ushahidi wa picha, na sisi Chadema tuna picha za mgombea wa CCM akiwa amevaa kufuli la mwanamke aliyefumaniwa naye, tuzioneshe kwa wananchi?
taratibu kidogo...twende tartibu....
Kwamba umesoma mwananchi ndo ukaja na hizi hoja, au hii ni habari kwenye gazeti la mwananchi?
Anyhow, ulichokiandika kina mashiko kwa sababu kama sasa tunakwenda kwa ushahidi wa picha, na sisi chadema tuna picha za mgombea wa ccm akiwa amevaa kufuli la mwanamke aliyefumaniwa naye, tuzioneshe kwa wananchi?
Kama mkakati wa kisiasa, CDM wakionyesha picha za mwana CCM akiwa kafumaniwa ni nzuri na itakuwa na impact kuliko wanayofanya CCM kuonyesha picha za Kada wao, tema DC, akiwa anaburutwa kama muhalifu. Technically CCM wanajionesha hawawezi kutawala mana kama Chama pinzani wana uwezo wa kumkamata DC kama mhalifu basi CDM ndio wana jeuri ya kuchukuwa madaraka.
Kwa mimi nadhani, CDM wangeweza kusambaza picha kama hizo za viongozi wa CCM wakiwanyanyasa wananchi, kwa jinsi wanavyolala bungeni, wanavyofuja mali za wananchi etc. CCM watachanganyikiwa mana wananchi watazidi kuamka!
Kwenye red: Nimeipenda hiyo na ndiyo maamuzi magumu yanayotakiwa -- yaani onyesho la uthubutu wa kufanya yale CCM huwa inashindwa kuyafanya hadi nchi hii inaenda hovyo hovyo.
chadema kwa kweli ni chama cha majambazi na wahuni, kamwe hawawezi kuchukua jimbo la igunga na wala nchi hii
Yessss....Chadamea nao wasambaze picha hizo za wanawake wajawazito wanaolala chini kwenye mawodi. Hapo CCM itakuwa imekwisha kabisa jeuri yake na itaangukia pua. Wezi na majambazi wakubwa, na ndiyo maana uchaguzi wa 2010 waliporomoka vibaya, wakaokoloewa na NEC.
kidumu chama cha mapinduziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.
Nakumbuka wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2010 kuna DC alilambwa mtama na kukwidwa na wanachama wa CCM wale waliomtenda DC huyo walichukuliwa hatua gani
Matendo madogo madogo yanayoigharimu CHADEMA, najua ni ushabiki tu, ila ndani yao nadhani wanajuta kwa ujinga huu, gharama yake ni kubwa mno. Viongozi wa CDM wanashaurika, juzi Mheshimiwi Lissu alikaa na wazee kutafuta jinsi kusafisha sura ya chama mbele za wananchi hasa Igunga...ninyi wapuuzi endeleeni kujifurahisha na ujinga wenu.