MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,966
CCM kubalini kua mlishashindwa hata kabla ya uchaguzi kurejelewa, kitendo chenu cha kuteua watu ambao waliyaachia majimbo kwa hiyari zao wenyewe bila hata ya kohombezwa na mtu halafu baada ya muda mfupi tu mnawalazimisha kurudi kuomba kura warudi tena kuyawakilisha majimbo hayo sio vyema hata kidogo. Hii haiingiu akili, wananchi hawawezi kuwaelewa kubalini kua mlishapoteza. Wananchi hawawezi kua wajinga kiasi hicho.
Mnawarudisha watu waliokataa ubunge waliopewa na wananchi, mmeambiwa wanchi wanawahitaji tena?
Majimbo mnayarudisha upinzani ninyi wenyewe na wala sio wananchi. Ni imani yangu kwamba hata kura za maoni zingefanyika kama zilivyo taratibu za kawaida kwenye chama, Dr Moleli na Maulidi Mtulia wasingepita wallah nawaambieni. Msiwalazimishe wananchi kufanya dhambi wasiyoipenda kwani maamuzi ni yao na wako huru kuamua nani awaongoze.
Sio tatizo kwani Majimbo ya Siha na Kinondoni yakirudi upinzani hamtapoteza kitu bungeni, upinzani utarudisha majimbo yao na CCM ridhikeni na lile jimbo la Longido mliloachiwa bure na yale mengine mliorudisha kule Singida Kaskazini na Songea.
Naomba amani itawale kwenye kwenye chaguzi hizi, acheni wananchi waamue mwenyewe.