CCM Kigoma yawafukuza wanachama 25 kwa kuwasaliti kipindi cha Uchaguzi

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,879
6,356
Chama cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Kigoma kimewafukuza uanachama 25 wa chama hicho baada ya kukisaliti chama kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Okt0ba 25 Mwaka jana.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kwenye ukumbi wa CCM Mkoa Katibu wa CCM mkoa wa Kigoma Naomi Kapambala alisema kuwa uamuzi huo wa kuwafuata uanachama ulitolewa na kikao cha halmashauri kuu cha Mkoa kilichofanyika tarehe 2 march mwaka huu.

Naomi alisema kuwa baaada ya uchaguzi mkuu kufanyika chama kilianza kufanyatathimini na changamoto walizokutana nazo kipinchi cha uchaguzi mkuu.

''Kwenye tathimini yetu hiyo tuliweza kugundua kuna baadhi ya wanachama ambao walikuwa siyo waaminifu kipindi cha uchaguzi mkuu walikuwa wakikisaliti chama tena wengine walikuwa viongozi na wengine waliogombea ubunge na kushindwa kwenye kura za maoni tumeamua watupishe sisi tuendelee kutekeleza ilani ya chama''alisema Kapambala.

Aliwataja wanachama waliofukuzwa uanachama kuwa ni pamoja Venance Mpologomi,Paul bahinda, Damasi Shetei,Gidioni Bunyanga,Edger Mkosamali,Pili Waziri,Pendo Jumanne,Robinson Lembo na Juma matete.

Wengine waliofukuzwa uanachama ni Idd Lugundanya,Juma Kifuku,Edga Bisoma,Staphord Kumuhanda,Jenoveva Bisana,Salehe Anatori,Abdallah Chugu,Atanas Andrea,Bigilimana Vyanda,Jonas Kafyiri,Isack Braytony,Christopher Chiza,Fanuel Kasogota,Laulent Bikulamuchi,Ibramu Shikuzilya na Paul Chabandi.

Alisema wanachama hao walifukuzwa uanachama wa chama cha mapinduzi tayari wameshahamia vyama vingine pia tathimini ya uchaguzi Mkuu bado inaendelea.

Naye Katibu wa jumuiya ya wazazi Mkoa wa Kigoma Staney Mkandawile alisema kuwa sasa hivi kazi iliyopo ni kutekeleza ilani ya chama na kuumunga mkono Rais John Magufuli kauli mbiu ya hapa kazi tu.

''Chama hakitamuonea mtu yeyote,ni bora tubaki wachache ndani ya chama lakini tuwe tunatekeleza ilani ya chama na kukipenda chama"Alisema Mkandawile
 
Na Christopher Chiza??????? au siye yule waziri wa Kilimo awamu ya nne?
 
Kuna jina limenistua, Christopher Chiza ni Waziri wa zaman au jina limefanana tu?
 
Ingekuwa chadema ndio imeita watu wasaliti na kuwatimua, watu hapa povu lingewatoka kama wamelishwa omo tangu utoto, ila ccm na nyie acheni kuonea vidagaa, huko makao makuu mbona hakunaga kufukuzana? mnatishiana tu vua gamba, vua gamba acheni kuonea wanyonge baada ya kuwatumia.
 
Chama cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Kigoma kimewafukuza uanachama 25 wa chama hicho baada ya kukisaliti chama kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Okt0ba 25 Mwaka jana.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kwenye ukumbi wa CCM Mkoa Katibu wa CCM mkoa wa Kigoma Naomi Kapambala alisema kuwa uamuzi huo wa kuwafuata uanachama ulitolewa na kikao cha halmashauri kuu cha Mkoa kilichofanyika tarehe 2 march mwaka huu.

Naomi alisema kuwa baaada ya uchaguzi mkuu kufanyika chama kilianza kufanyatathimini na changamoto walizokutana nazo kipinchi cha uchaguzi mkuu.

''Kwenye tathimini yetu hiyo tuliweza kugundua kuna baadhi ya wanachama ambao walikuwa siyo waaminifu kipindi cha uchaguzi mkuu walikuwa wakikisaliti chama tena wengine walikuwa viongozi na wengine waliogombea ubunge na kushindwa kwenye kura za maoni tumeamua watupishe sisi tuendelee kutekeleza ilani ya chama''alisema Kapambala.

Aliwataja wanachama waliofukuzwa uanachama kuwa ni pamoja Venance Mpologomi,Paul bahinda, Damasi Shetei,Gidioni Bunyanga,Edger Mkosamali,Pili Waziri,Pendo Jumanne,Robinson Lembo na Juma matete.

Wengine waliofukuzwa uanachama ni Idd Lugundanya,Juma Kifuku,Edga Bisoma,Staphord Kumuhanda,Jenoveva Bisana,Salehe Anatori,Abdallah Chugu,Atanas Andrea,Bigilimana Vyanda,Jonas Kafyiri,Isack Braytony,Christopher Chiza,Fanuel Kasogota,Laulent Bikulamuchi,Ibramu Shikuzilya na Paul Chabandi.

Alisema wanachama hao walifukuzwa uanachama wa chama cha mapinduzi tayari wameshahamia vyama vingine pia tathimini ya uchaguzi Mkuu bado inaendelea.

Naye Katibu wa jumuiya ya wazazi Mkoa wa Kigoma Staney Mkandawile alisema kuwa sasa hivi kazi iliyopo ni kutekeleza ilani ya chama na kuumunga mkono Rais John Magufuli kauli mbiu ya hapa kazi tu.

''Chama hakitamuonea mtu yeyote,ni bora tubaki wachache ndani ya chama lakini tuwe tunatekeleza ilani ya chama na kukipenda chama"Alisema Mkandawile

  • Hii inaweza kuwa mwendelezo wa awamu ya visasi
  • Lakini nimesikia mwenye kaya amesema mambo ya vyama yamekwenda likizo anachoangalia ni mahitaji ya raia wake
  • Huyu Venance Mpologomi ni yule wa kashfa ya minofu ya samaki enzi za Mkapa kama si Mwinyi?
 
Nina wazo wakuu.....

Inanzishwe thread ya watu wanaofukuzwa.....! Kwa muhula Wa kwanza Wa JPM
Hao watu walishahama ndani ya chama toka enzi ya dhoruba ya Lowasa wakuu.Mimi ni ccm,lakini sitakaa niisahau ile dhoruba kwani ilisomba kuanzia vijidagaa mpaka papa na nyangumi
 
Robson Lembo huyu amefukuzwaje wakati aligombea ubunge kupitia CHAUMA jimbo la Kigoma kaskazini.Au sio yeye?.
 
Edger Mkosamali alikuwa mgombea ubunge(ACT), BUNYAGA mgombea ubunge nccr (kasulu mjini) walishakiacha Chama chaccm kitambo
 
Hao watu walishahama ndani ya chama toka enzi ya dhoruba ya Lowasa wakuu.Mimi ni ccm,lakini sitakaa niisahau ile dhoruba kwani ilisomba kuanzia vijidagaa mpaka papa na nyangumi
Hahahah aisee mjapan mweusi unanichanganya ,kuna sehemu umekana kwamba wewe sio ccm na haitakaa itokee hivyo ,huku tena wewe ni ccm
Nanukuu ... Personally I'm not ccm, and I'll never be. But i don't support this thread. President of Tanzania is a tanzanian for tanzanians and our language is one, Swahili.
 
Mnamfukuzaje mtu aliyekwishajiondoa? Naona kuna file linatakiwa kujazwa hapa kupelekwa makao makuu vinginevyo sioni logic ya mtu kufukuza mtu aliyekwishajiondoa. Naona ndani ya hiyo system bado kuna kuogopana...kwanini msitimue walioko sasa ambao walikuwa wasaliti? Ina maana waliisha?
 
CCM wahuni tu kama Rais wao!Robson Lembo alitangaza kuondoka CCM mwezi August mwaka jana na akagombea hadi ubunge kupitia upinzani lkn eti leo anafukuzwa

Yale yale ya hakuna kuchangia elimu lkn sasa tunachangia
 
Mnamfukuzaje mtu aliyekwishajiondoa? Naona kuna file linatakiwa kujazwa hapa kupelekwa makao makuu vinginevyo sioni logic ya mtu kufukuza mtu aliyekwishajiondoa. Naona ndani ya hiyo system bado kuna kuogopana...kwanini msitimue walioko sasa ambao walikuwa wasaliti? Ina maana waliisha?
Cku hizi kutimua ndo dili kwa ccm wakiishiwa hao wa kuwatimua watahamia majumbani kwao c unajua utamu wa nyama ya mtu so mahausigel wajiandae
 
Back
Top Bottom