Ccm kama farao wa misri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm kama farao wa misri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MGOGOHALISI, Apr 24, 2012.

 1. MGOGOHALISI

  MGOGOHALISI JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 353
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Siwezi shangazwa na tabia ya serikali iliyoko madarakani kuendelea kufanya makosa na kutowajibika kwa viongozi husika. Hii inanikumbusha habari za wana wa Israeli walipokuwa utumwani enzi zile(Kutoka 3:7-10). Baada ya Mungu kuona mateso ya wana wake alimtuma Musa kwa Farao( Kut. 3:10). Lakini farao alikua na moyo mgumu asitake kuwaruhusu wana wa Israel watoke Misri. Licha ya mapigo mengi aliyoyatoa, bado farao aliendelea kuwa na moyo mgumu wa kutosikia.( Kama ccm sasa hawasikii la mtu, wanaendelea kufanya makosa). Lakini mwisho wa siku wana wa Israel walitoka Misri tena kwa Jeuri( Kut.35-36). Watanzania wamekua mateka kwa mafisadi wa ccm kwa muda mrefu. Ukombozi wao umekuja japo CCM(Farao) bado anaonekana mgumu kutoa haki. Ila tusife moyo, hizi ni hatua za mwisho za ccm kutawala, siku chache zijazo itapigwa pigo la mwisho na haitainuka, mafisadi wote tutawateka na kuchukua kila tunachotaka maana watakua hawana ujanja. CCM itaendelea kufanya makosa hadi ife iangamie, tusitarajie mazuri yoyote kutoka kwao kwani laana imeshawashukia kwa dhuruma waliowafanyia watanzania. Mungu amewafanya wawe vipofu na viziwi wa vilio vya watanzania(Kama farao alivyofanya kwa Wamisri) Ili hata wananchi wanaodanganywa kwa kofia na fulana waamke na kuichukia, hatimaye itaangukia pua katika uchaguzi maana hao ndo tegemeo lake. Mwananchi wa kawaida kabisa anategemea serikali itatue kero zinazomzunguka kwa kodi anazolipa, lakini ccm wanazitumia kununua mashangingi.H akika anguko la ccm limefika. Hawatakua na jema kwetu tenna la kutufanya tuwaangalie. R.I.P CCM!!!!
   
Loading...