Kuna kila sababu kwa Chama cha Mapinduzi kujitokeza hadharani kulaani ufisadi na ubadhirifu mkubwa wa mali za umma uliotawala katika Halmashauri karibu zote hapa nchini ambapo miradi mingi imesimama hasa ya Vituo vya Afya na Sekondari Mpya.
Mbunge wa Buchosa, Erick Shigongo amesema kwenye jimbo lake hela zimeliwa miradi yote ya vituo vya afya imesimama
"Nakuomba Kaka yangu, Mh Kassim Majaliwa
@kassim_m_majaliwa, Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uje Buchosa ujionee, vituo vya afya vya Maisome na Nyanzenda havijakamilika pesa zimeliwa na kazi haijaisha" ameandika Shigongo
Ni muhimu sasa CCM kujitokeza hadharani kulaani ufisadi huu