CCM Jimbo la Ukonga Takrima nje nje

CCM Jimbo la Ukonga Takrima nje nje

Chipoku

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2011
Posts
254
Reaction score
181
Mh Meya mstaafu kashaanza kutoa takrima kwa Wenyeviti wa Kata katika Jimbo la ukonga kama kawaida yake . Njooni Ukonga mfaidi tu.

Mwanzoni mwa wiki hii Jerry Slaa alikuwa na Kikao na Viongozi wa CCM Kata za Buyuni na Pugu. Kikaoni kulikuwa na wajumbe 20 na kila mmoja aliondoka na 30,000/= ili wasije kumwangusha wakati wa kura za maoni ndani ya Chama.

Huko Kata ya Kivule Werema nae hakubaki nyumba, amefanikiwa kukutana na viongozi wa Kata hiyo pamoja na mitaa yake na wahudhuriaji wakafanikiwa kuondoka na 20,000/= kila mmoja.

Huku Jeri Slaa alipata utata baada ya mjumbe mmoja (mwakilishi wa wazaxi wilaya) kukataa kitita na kuahidi kulipeleka suala hili CCM Wilaya Ilala.

Ngoja tuone nani ni nani!
 
Jerry silaa amekomaaa na Ukonga kwelikweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukonga yenyewe hii hasa hapa buyuni penyewe kwenda hadi kwenye jenga uza maarufu kama nyumba za mchini hadi mradi wa viwanja elf20 basi utazani hapajawahi kuwa na uongozi ndani ya miaka 15 iliyopita!! Ni shida barabara hakuna Karisa. Ukitembea na gari kule siku mbili basi una moyo mgumu juu ya gari.

Pale Italian kuna milory inafanya kazi ya kutifua na kujaza tope barabara hakuna kazi inayoonekana ikifanyika. Hakaki kama watu wote wa Ukonga wangekuwa waelewa, wangegoma kuchagua mpaka miundo mbinu (hasa barabara na umeme) vya eneo la ukonga kwa ujumla vipewe kipaumbele cha kuridhisha.
 
Ukonga yenyewe hii hasa hapa buyuni penyewe kwenda hadi kwenye jenga uza maarufu kama nyumba za mchini hadi mradi wa viwanja elf20 basi utazani hapajawahi kuwa na uongozi ndani ya miaka 15 iliyopita!! Ni shida barabara hakuna Karisa. Ukitembea na gari kule siku mbili basi una moyo mgumu juu ya gari. Pale Italian kuna milory inafanya kazi ya kutifua na kujaza tope barabara hakuna kazi inayoonekana ikifanyika. Hakaki kama watu wote wa ukonga wangekuwa waelewa, wangegoma kuchagua mpaka miundo mbinu (hasa barabara na umeme) vya eneo la ukonga kwa ujumla vipewe kipaumbele cha kuridhisha.
Unaonekana unatumia nguvu nyingi sana kwenye kuandika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uite watu waache kazi yao ya pesa yakula sikuhiyo uwakalishe masaa waskilize yako alafu watoke bila hata nauli ya bodaboda ama tax huo si upuuzi! Msimezeshwe maujinga ya kiwivuwivu pesa kidogo yakujikimu siyo rushwa huo ni ukarimu unaostahili kufanywa!
 
uite watu waache kazi yao ya pesa yakula sikuhiyo uwakalishe masaa waskilize yako alafu watoke bila hata nauli ya bodaboda ama tax huo si upuuzi! Msimezeshwe maujinga ya kiwivuwivu pesa kidogo yakujikimu siyo rushwa huo ni ukarimu unaostahili kufanywa!!
Ndivyo ilivyo andikwa kwenye katiba ya CCM?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom