CCM itavuka salama kufika 2015?

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Messages
4,021
Points
1,250

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined May 26, 2009
4,021 1,250
NA MASHAKA MGETA

22nd November 2012

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepitia hatua tofauti ndani ya takribani 12, kikilenga kujisafisha na kurejesha kukubalika zaidi kwa jamii.


Wapo wanaoamini kwamba CCM imepoteza mwelekeo. Unapolizungumzia hilo, wahafidhina na wanaojikomba kwa chama hicho wakiyaelekea mahitaji na maslahi binafsi, wanakuweka katika kundi la ‘wapinzani'.

Lakini ukweli unabaki kuwa, CCM ya sasa si CCm ya kuanzia Februari 5, 1977 hadi kabla ya mchakato wa kumpata mgombea urais kupitia chama hicho mwaka 2005.

Lugha ya ‘sisi CCM' hivi sasa haipo, imebaki kuwa ‘wao' na ‘sisi'…ndani ya chama kimoja, chenye dira moja, mwelekeo mmoja na malengo yale yale!

Itakumbukwa kuwa baada ya ‘ushindi wa kishindo' katika Uchaguzi Mkuu wa 2005, CCM ‘ilifumua' safu ya uongozi wake. Hapo ndipo hatari ilipoanzia.
Viongozi shupavu kama aliyekuwa Katibu Mkuu wake, Philipo Mangula, `walitupwa', nafasi yake ikachukuliwa na Yusuph Makamba.

Nafasi muhimu katika chama zikatolewa kwa upendeleo. Waliokadhibiwa nafasi hizo hawakuwa na mamlaka za kimaadili, bali kutimiza matakwa yao.

Katibu wa Fedha na Uchumi akapewa Rostam Aziz, mfanyabiashara ambaye hakuwa kivutio kwa chama, wanachama na umma.
Wakati hali ikiwa hivyo, CCM ikajikita katika makundi, yakiwa yameasisiwa na waliokuwa pamoja katika kutafuta uongozi wa nchi, waipate nafasi ya Urais.

Kwa vile dhamira ya makundi yaliyojijenga katika taswira ya mtandao, ilikuwa kuingia Ikulu, (pengine) wasijue wakiingia huko watafanya nini, hawakudumu katika umoja wao.

Inawezekana na kutokana na ushahidi wa kimazingira, walikuwemo miongoni mwa wana mtandao, waliokusudia kuyasimamia mambo mema na adilifu kwa chama na nchi.

Lakini wakakinzana na kikundi kidogo chenye nguvu ya fedha, kikinuwia ‘kuitafuna' nchi, ikibidi ibaki ‘mifupa mitupu!'
Mzigano wa fikra na matamani yao yakazidisha nguvu za mpasuko ndani ya kundi ambalo lengo kuu lilikuwa kuingia Ikulu…basi!
Hata sasa makundi hayo yanazidi kutanuka. Wana-CCM wa kundi hili wanawasamaka wa kundi lile. Kila mtu ana sharubu! Kuviambiana, kukashifiana, kukejeli na aina nyingine za uovu dhidi ya maadili na uwajibikaji wa pamoja.
Mabadiliko yalipofanyika hususani katika sekretarieti iliyoongozwa na Katibu Mkuu, Yusuph Makamba, Wilson Mkama na wengine wakachaguliwa.

Lakini kwa kipindi chote, Mkama akawa ‘yupo kama hayupo', shughuli nyingi za CCM kwa umma zikafanywa Katibu wa Uenezi na Itikadi, Nape Nnauye.
Nape anajulikana ndani na nje ya CCM, yupo katika kundi linalowapinga viongozi na wanachama wanaotuhumiwa kwa rushwa na ufisadi.
Amezunguka sehemu kubwa ya nchi akihubiri habari ya ‘kujivua gamba', lengo likiwa kuwadhibiti ‘magwiji' wa rushwa na ufisadi ndani ya CCM.

CCM ikazidi kuyumba, ikazidi kupata mtetemeko. Kwa maana kundi linalosomamia maadili, likazidi kupambana na wanaoyakiuka maadili, wakituhumiwa kwa rushwa na ufisadi.
Hata chama kilipoundwa kamati iliyoongozwa na Rais mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, ishughulikie mpasuko na kurejesha umoja ndani ya chama hicho, ni sawa na kusema ‘hakuna kilichofanyika.'

Mkama ametoka na kutoa mwanya kwa Abdulrahman Kinana na wajumbe kuingia katika uongozi wa CCM.
Wakiwa katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam, ‘viongozi wapya' wa CCM wakaendeleza baragumu lenye mlio wa kuwashughulikia ‘magwiji' wa rushwa, wanaotajwa kushinda nafasi tofauti za uchaguzi uliomalizika hivi karibuni.
Kwa maana nyingine, sauti iliyosikika kutoka kinywani mwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye, kuhusu mafisadi, bado inapazwa, ienee.

Ni mwelekeo ule ule wa kushamirisha makundi, wanaojinasibu kwa kupiga vita ufisadi na wanaokumbatia kashfa za ufisadi, wakitumia fedha kununua uongozi.

Tujiulize, CCM itavuka salama daraja la mgawanyiko uliojikita ndani yake, ili ukifika wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2015, kiwe salama kushiriki na kushinda?
Kwa maana kinachoonekana sana kwa CCM, viongozi na wanachama wake ni maneno matupu yasiyoweza kuvunja mifupa.
Viongozi wenye dhamana wanaonya, wanakaripia, wanaelimisha, wanafanya kila jitahada, ambavyo hata hivyo vinakuwa mfano wa kumpigia mbuzi gitaa.

Lipo tatizo ndani ya CCM, chama ninachokijali kwa vile kina watu, kina umma, kinatumia rasilimali za umma kama vilivyo vyama vingine vya siasa.
Lakini kubwa zaidi CCM ni chama kilichoshinda Uchaguzi Mkuu wa 2010 na kuunda serikali, hivyo hakipaswi kudharauliwa. Kinastahili kujadiliwa.

Haiwezekani CCM ikavuka salama daraja la mgawanyiko huo kupitia ‘huyu ni mwenzetu' na ‘yule ni wa kule'. CCM inapaswa kurejea, kiwe chama kimoja chenye watu wamoja wanaonuia dira na mwelekeo mmoja.
Si Mangula, si Kinana si awaye yote anayeweza kuleta mageuzi yenye matokeo chanya kwa CCM isipokuwa kubadili mfumo ulioasisi na kusababisha chama hicho kubadili mwelekeo wake.

CCM inapaswa kurejea dhamira yake kwa kadri inavyoainishwa kwenye alama za jembe linalowawakilisha wakulima na nyundo, ikiwalenga wafanyakazi.

Chama kirudi kwa umma unaoundwa kwa asilimia kubwa na wakulima na wafanyakazi na si kuwakumbatia matajiri waliokaribishwa, wakaingizwa, lengo lao likiwa ni kuficha uovu na kupata fursa pana ya kushiriki uovu zaidi.
Itakapofikia hatua hiyo, CCM kitakuwa chama salama, vinginevyo umma utawaadhibu watakapoingia katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, kwa maana ‘wamekalia' makundi badala ya kushughuli kero za umma, maendeleo na ustawi wa watu.

Mashaka Mgeta ni Mhariri wa Makala wa NIPASHE Jumapili. Anapatikana kupitia simu namba +255 754 691540 ama barua pepe: mgeta2000@yahoo.com.
CHANZO: NIPASHE


 

Kiona

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2012
Messages
934
Points
195

Kiona

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2012
934 195
CCM ipi mnayoizungumzia?? kama ni hii yenye viongozi wasiyo waadilifu sahauni.

Ikiwa Raisi Obama amekaa madarakani miaka minne na kufanya jumla ya safari 32 alitakiwa kutaja faida ya kila safari ili apate uhalali wa kuchaguliwa tena na alieleza na akaeleweka mbele za wapiga kura na kuchaguliwa tena. Nyerere alikaa ikulu miaka 24 almost 25 na alifanya jumla ya safari 68 tu na alijenga viwanda na kuanzisha mashirika ya umma yasiyo na idadi. Mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais wa sasa wa Tanzania amekaa madarakani kwa miaka 6 na kufanya jumla ya safari zaidi ya 322 na ukimuuliza nini manufaa ya safari hizi sijui kama kuna jibu la kueleweka. Sasa kwa takwimu hizi CCM watatuambia nini?

Labda watanzania tusaidiane mawazo ni nini kifanyike kudhibiti mfumko wa safari kwa Raisi wetu kwenye nchi masikini kama yetu na umaskini wenyewe ni wa kujitakia. Katibu mkuu mwenyewe kutoka CCM naye anamiliki kampuni ya kusafirishia hata kautajiri kale kadogo alikotupa mwenyezi Mungu. Meno ya tembo na wakiisha nafiri tutasafirishwa sisi.

Tunavyoendelea hawa walafi kuna siku wataanza hata biashara kuuza figo za watanzania nje.

povu linanitoka hapa
 

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Messages
5,141
Points
1,500

kbm

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2012
5,141 1,500
Tatizo viogozi wetu karibia wote ni wagonjwa..., naona kama akili zao hazifanyikazi vizuri...
 

Kimagege

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2010
Messages
283
Points
195

Kimagege

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2010
283 195
huy mgonjwa anakufa ndugu yangu.huitaji kupewa udakta wa kichina kama wa mkuu wa kaya ili kujua hilo.kwa sasa huyu mgonjwa anatupa mikono na miguu kama atarudi kumbe ndo anakufa.
 

malaka

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2012
Messages
1,326
Points
1,195

malaka

JF-Expert Member
Joined Apr 5, 2012
1,326 1,195
Bado mnakiombea dua hiki chama hamani? Hapo ndio ntoleeeni hiyo. We pata picha tu hali halisi ya sasa. Labda 2015 watumie Jeshi sio polisi au UWT.
 

Forum statistics

Threads 1,392,370
Members 528,604
Posts 34,106,922
Top