CCM itatoka madarakani endapo upinzani utafanya haya

mpenda1961

Senior Member
Apr 2, 2013
123
78
1.Kujitofautisha na CCM

Upinzani umekuwa ukifanya mara nyingi mambo ambayo CCM inafanya

2. Kuwa na agenda ya kudumu

Upinzani haijawahi kuwa na lengo kuu au mkakati ambao walianzisha ukafikia mwisho kama M4C ilivyopotea, naamini kama M4C ingeendelea kwa moto ule ule ulioanzia basi uchaguzi uliopita ungekuwa mwepesi sana.

3.Kuacha kutegemea wanaokimbia CCM

Hii ni ishara kwamba upinzani hauna hazina ya viongozi waliowaandaa kushika nyadhifa kubwa kutoka ndani ya wanachama wake.

4.Kuandaa mfumo mzuri wa kuachiana madaraka

Hili ni tatizo kubwa kwa vyama vyote vya upinzani, wenyeviti wengi wamefanya vyama kama mali zao kitu ambacho kinawafanya watanzania kutokuamini upinzani 100%.

6. Kukubali challenge

Vyama vingi vya upinzani havikubali kukosolewa na wanachama na kila anayekosoa lazima ataundiwa zengwe, hii ipo mpaka CCM pia.

7. Kuacha kupeana nyadhifa kama fadhila.

Hili limekuwa tatizo kubwa sana kwa vyama vyote, kupeana madaraka kwa kujuana na sio uwajibikaji wa mtu.

8.Upinzani uache kucheza ngoma ya CCM

Kikubwa vyama vya upinzani vijitahidi kujenga mifumo imara ya vyama kuliko watu watiifu kwa viongozi wakuu wa vyama, hii inajitokeza kwa vyama vyote kwa viongozi kuweka vibaraka wao ipo kwa wenyeviti wote wa upinzani mbowe, Mbatia, Zitto na hata Seif.

ASANTENI
 
Back
Top Bottom