CCM itaruhusu mgombea ndani ya chama uchaguzi ujao?

mkafrend

JF-Expert Member
May 12, 2014
3,047
1,503
Wanaccm, salaam!

Kwa kawaida nafahamu kuwa rais anayetokana na chama cha mapinduzi anapokuwa akiongoza muhula wa kwanza wa urais huwa makada wengine hawaweki nguvu za kutosha kusaka nafasi hiyo. Hata hivyo katiba ya nchi na chama vinaruhusu. Iliwahi kutokea sitofahamu kwa mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la MPENDAZOE alipotangaza kwamba angegombea urais mwaka 2010; hapa lilifuata tifu kubwa na kufukuzwa uanachama ndani ya CCM.

Leo miaka takribani saba au nane baada ya tukio hilo napenda kufahamu iwapo ni uvunjaji wa kanuni, sheria na taratibu kwa mwanaccm kuchukuwa fomu ya kusaka kuteuliwa na chama ili apeperushe bendera katika uchaguzi ujao. Hapa naomba michango ya mawazo na yasiwe matusi wala dhihaka.

UHURU WA MAONI; UHURU WA MAWAZO
MUNGU IBARIKI TANZANIA - MUNGU MUBARIKI JPM
 
Kama utakuwa ulimsikiliza na kumuelewa vizuri Bulembo juu ya uchaguzi wa tar. 23 natumaini jibu utakuwa nalo.
 
Cheo cha mwenyekiti wa CCM taifa hugombewa.Na ni ruksa kila mwanachama yeyote kugombea.Process ya kumpata mwenyekiti wa CCM huanzia kuchukua fomu ya Uraisi.Hivyo hata wewe na Mpendazoe wako na yeyote awaye kama kweli una nia au ulikuwa na nia ya kuwa mwenyekiti wa CCM ilibidi uchukue fomu ya kugombea uraisi kama wale wengine kibao akiwemo yule mkulima toka kigoma ambaye ni darasa la saba alivyokuwa kapania kugombea uraisi ili baadaye aje awe mwenyekiti wa CCM taifa.

Fomu za kugombea uraisi ndani ya CCM hutolewa kwa yeyote mradi ni mwanachama hai.
 
Hiyo sio mila na si utamaduni wa chama, asubiri baada ya miaka kumi vinginevyo huko kutakuwa ni kukibomoa chama
 
Leo miaka takribani saba au nane baada ya tukio hilo napenda kufahamu iwapo ni uvunjaji wa kanuni, sheria na taratibu kwa mwanaccm kuchukuwa fomu ya kusaka kuteuliwa na chama ili apeperushe bendera katika uchaguzi ujao.

Chama huwa kina utaratibu wake muda ukifika wa uteuzi wa mgombea wa CCM .Hatuna utaratibu kama wa CHADEMA ambapo Lowasa ameshatangaza atagombea 2020.Chama hutoa mwongozo ,ratiba na kila kitu.Ukianza kujitangaza mapema kabla ya filimbi ya Chama kuruhusu utashughulikiwa na chama.Kama utakumbuka wengi waliadhibiwa kwa kuanza kampeni ya kutaka wachaguliwe kugombea kabla ya muda.Subiri muda ufike Chama kitoe mwongozo.Kwa sasa tulia ni hapa kazi tu hadi 2020.Ukifika wakati huo chama kitakueleza kila kitu.Kwa sasa tuwaachie akina Lowasa ambao wameshajiteua kuwa wagombea uraisi 2020 bila kupitishwa na kikao chochote cha CHADEMA wala UKAWA
 
Mpendazoe hakuwai kutangaza kugombea Urais acha upotoshaji usio na maana yoyote, Mpendazoe aliandika Makala katika gazeti la Raia Mwema kukosoa utaratibu wa kushughulikia mafisadi ndani ya Chama cha mapinduzi ambae Mwenyekiti ni JK..

Akapata tetesi kua katika mkutano mkuu unaotarajiwa kufanyika angefukuzwa uanachama, akaamua kujiuzuru Ubunge, na kuhama Chama, sababu mda ulikua umeshaisha, mda si mrefu kufanyika uchaguzi mkuu.. Hivyo Jimbo Lake likabaki wazi, Jimbo la kishapu la mbunge shapu - Nchambi

Hivyo basi alihamia Chama kilichokosa nguvu CCJ na kudai wenzake wanakuja, ila hawakuenda, a kaamua kuhamia Chadema, akapewa Jimbo la segerea.. Ambapo alimtikisa kwa nguvu sana Mahanga
 
Back
Top Bottom