Kitaja
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 2,836
- 1,383
Wana JF salaam,
Katika pilika pilika zangu za kikazi nimefanikiwa kutembelea mikoa mingi ya nyanda za juu kusini ikiwemo Iringa, Njombe, Mbeya, Rukwa na Katavi. Katika sehemu zote nilizopita niliona mwitikio mkubwa wa kutaka mabadiliko kutoka UKAWA. Nilishangaa hata ile mikoa iliyokuwa ni ngome ya CCM kama Rukwa na Katavi lakini upepo umebadilika sana wimbo ni ukawa tu kwa akina mama na vijana. CCM wanajitutumua lakini hawana mvuto tena.
Nikiwa mkoani Mbeya nimeshuhudia uzinduzi wa kampeni za CCM na UKAWA. Wilayani kyela Mwakyembe hana chake japo anatumia nguvu kubwa ya dola na propaganda za magazetini. Wilayani Rungwe, jimbo la Prof. Mwakyusa linachukuliwa na UKAWA bila kuuliza. Nilipita Mbozi na baadaye Momba kwa hakika Silinde anachukua kirahisi jimbo hili.
Mbeya mjini, Sugu hana mpinzani na nimewasikia wana CCM wenyewe wakionekana kukata tamaa. Nilifanikiwa kufanya mazungumzo na baadhi ya wana CCM ambapo mzee mmoja maarufu hapa mbeya anayemiliki mabasi kadhaa ya abiria alikiri kuwa CCM ni maji ya shingo mwaka huu hasa kwa nafasi ya urais. Tatizo kubwa alisema ni timu ya kampeni kusheheni watu wasio na uwezo. Na kingine aliponda mtindo wa kuwatumia wasanii toka Dar wakati mikoani pia kuna wasanii tena wenye uwezo mkubwa.
Jambo lingine japo sikukubaliani naye mzee huyu maarufu mkoani mbeya alidai CCM wana matumaini ya kushinda ubunge mwaka huu. Kigezo alichotumia ni ukabila. Anadai kwa sasa wanyakyusa na wasafwa wameungana kumpinga Sugu ambaye ana asili ya ukinga japo amezaliwa na kukulia mbeya. Mimi si shabiki wa siasa za ukabila na nina uhakika wana mbeya wengi hawako hivyo ndiyo maana walimchagua Sugu kwa kishindo 2010 na sasa wanaenda kufanya hivyo. Nilishuhudia kampeni za Shitambala maeneo ya Mwanjelwa hakubaliki kabisa licha ya vitisho vingi walivyovitoa kwa wapinzani wao lakini umma ulionyesha mapenzi yao ni chadema/ ukawa. Mkutano wote ulilipuka kwa shangwe pale gari la kampeni la chadema lilipopita maeneo hayo na kuwafanya CCM wazidi kuwa wanyonge, kwa kweli kampeni zao ziliisha vibaya.
Kwa mwendo huu, CCM wajiandae kukabidhi dola kwa amani, sioni namna watakavyoepuka kikombe hiki.