CCM itachukua nchi 2015?

CCM itachukua nchi 2015?

loisaibulu

Member
Joined
Mar 20, 2014
Posts
9
Reaction score
0
Kuna wanaoamini kuwa mwisho wa ccm ni mwaka 2015. Hao wanajidanganya lakini lolote laweza kutokea watanzania. Hakuna dalili kuwa chama cha mapinduzi kitapoteza kiti chake cha urais kwa mara ya kwanza. Ni vigumu sana. Unajua ugumu uko wapi? Watanzania wengi bado wana imani na chama hiki kukongwe nchini kuliko xote. Pia watanzania wengi huogopa sana pilikapilika za mabomu na risasi ktk machafuko. Ccm inategemea jshi la.police kushinda. Mathalan Chadema imepata nguvu hasa ktk kata na ubunge. Kuna uwezekano rais kutoka ccm na wabunge wa chadema kuwa wengi
 
Ikulu ni mahala pa takatifu, katu haiwezi kukanyagwa na wapinzani hasa chadema, wananuka damu
 
Unauliza unachojua au unataka kujua zaidi nani hajui kuwa ccm ni chama pendwa kinachowakilisha watanzania wote bila ya ubaguzi.
 
Hatujawa na chama cha upinzani chenye uwezo wa kuongoza taifa vyama vyote vilivyopo kwa sasa havijafika hatua hiyo kwa sasa.
 
Vyama vya upinzani viongozi wao wakiacha uroho wa madaraka na kukubaliana kuweka mgombea mmoja tu badala ya kila chama kuweka mgombea wake, basi chama cha majambazi kitakufa kifo cha mende miguu juu. Na ikiwa wapinzani wataendelea kuweka kila chama mgombea wake basi majambazi watatawala kwa muda mrefu. Wapinzani waige Kenya, walifanikiwa kuweka nguvu moja na kung'oa KANU. Kila jambo linawezekana.
 
Ikiwa CCM hawatachakachua kura tena 2015, uhai wao utakuwa umefikia tamati. Ila tatizo ni kwamba kwa kuwa magamba wameliteka bunge la katiba itakuwa vigumu kupatikana tume huru ya uchaguzi.
 
Unauliza unachojua au unataka kujua zaidi nani hajui kuwa ccm ni chama pendwa kinachowakilisha watanzania wote bila ya ubaguzi.

CCM ingekuwa inapendwa wasingekuwa wanaonga kanga,pesa,chumvi,na kununua kadi wakati wa uchaguzi.nyambafu.
 
we ucjal cc vijana tumeshaamua kuw ccm haikanyag ikulu we achana na hao wazee wenye iman kali bila kuangalia mabadiliko
 
Yaaani kweli unauliza vumbi stoo? ???
 
Back
Top Bottom