CCM inatupeleka wapi?

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
2,175
Reaction score
4,179
Ni sababu gani zimewafanya CCM kukimbilia kwenye vyombo vya ulinzi na usalama? Nini kimewakuta na kuwasibu ? Wanaitegemea Tume ya uchaguzi kuliko Mungu, wamehisi kitu gani?

Sasa niwaulize siku nayo ikifika vyombo hivi vikawageuka na kuwaepuka CCM ,yaani umefikia wakati wa vyombo hivi kuwaambia CCM wapigane na hali yao ,Je mwenyekiti wa CCM ambae ndie raisi ataivunja Tume na kuchaguzi ngingine?

Akuna asiejua na kuelewa kuwa hapa tulipofikia CCM imewekwa kwenye kona,wamebaki CCM watetezi ambao hawajai hata kiganja, mbinu na hila zao ni lazima wawatumie CCM wavaa sare tu, ambao ni wengi na wamo katika kupanga mipango yao miovu,ndio unakuta washiriki na njia zote ovu wanazozipanga zinakuwepo uwanjani,jambo ambalo linawatia dosari polisi na tume yenyewe.

Mwisho wa siku polisi wanasema ni amri kutoka juu, mwisho wa siku wanajitetea kuwa wanamlinda Tundu Lisu, Sasa sasa umefikia wakati polisi wawambie CCM watetezi tumieni vijana wenu wanaoogopa nyuki kwenye hio mipango yenu miovu, UVCCM ambao ni magoigoi kupindukia.

Kuna siku vyombo hivi vitawageukia CCM ni suala la muda tu, WaTanzania wa sasa ni bora wajifie kuliko kuendelea kuongozwa kimbuzi maisha ya vuta nikuvute, na hawa CCM watetezi wajijue wanahesabika na hawana nguvu ya kuushinda umma ,umma umebadilika sio ule wa piga tajame.

Hivi vyombo wanavyovitegemea CCM ni vyombo vya waTanzania wote katika mechi hii hawatakiwi kukingia kifua upande mmoja,mpaka wanaopachua bendera mnatumwa kuwalinda,mnatakiwa mmfanyiwe Upemba tu, maana Pemba UVCCM wamekoma kupachua bendera muulizeni Bashiru alipokwenda kwa kishindo Pemba alindoka na kurudi kimyakimya, unapachua bendera kwenye tawi la ACT, Wapemba wanakukamata hata kama kuna polizi na mizinga,wanakuvua suruali arafu wanakwambia potea haraka kabla hawajakunwea tende aka kangara.

Hapa Tanganyika naona bado mnawachekea UVCCM, mbele ya vyombo vya sheria na wao wanawajibika kama nyinyi ni aibu ya kimaaifa polisi kumlinda UVCCM kushusha bendera ya chama kingine au kuondoa picha za wagombea.

Mimi nawaomba tu UVCCM muache hio tabia anekutuma kama amekupa hela na kukunywesha temo ili kukuondoa akili,wewe hizo hela kula na mwambie ulipofika bendera hukuiona,asikutafutie kifo kwa maslahi yake.
 
Sasa umefika wakati wa kuheshimiana polisi wasiwaogope UVCCM,embu tuone polisi anajiuzulu kwa kukataa amri ovu za CCM .atakuwa shujaa wa kwanza kwa zama hizi hapa Tanzania.
 
Mfa maji!!! Hujaribu kuyashika akidhani ni kamba. CCM imesha jua Watanzania hawaitaki. Wamebaki kutumia silaha zao za mwisho.
 
Mimi sina chama ila naona CCM na Magufuli wanafanya kazi nzuri na wanapendwa sana
 
Polisi walio wengi hawaitaki CCM na wao mwezi huu kuna harufu nzuri sana kutoka kwao kuwa wanafanya kweli,mambo ya kugombanishwa na raia wameshayachoka,maana kadili wanavyojipamba bado wanaonekana wana sura mbaya mbele ya wananchi walio wengi,mbona zamanipolisi walikuwa ni friendly tu,sasa kila wanapopita wanaonekana kama wanyama pori jambo ambalo linawatia wasiwasi katika maisha yao ya kila siku na maisha baada ya saa za kazi.

Polis wameshaishtukia CCM kuwa inawatumia wakati huu wa uchaguzi na wakuu wachache wanabebwa na CCM kwa hali na mali ila walio wengi wanasema hila za CCM kuwaghilibu wakuu zinafahamika,na kura za mwaka huu zitawaumbua wanaotumika na ccm.
 
Octoba 30 mje tena muandike hivi hivi ccm ipo Monchwari
 
Imetutoa kwenye uchumi wa chini mpaka wa kati wa chini, Sasa funga mkanda maana nchi inakwenda kwenye uchumi wa kati wa juu. CCM chama bora kabisa, Magufuli Rais bora kabisa. Tanzania nchi bora kabisa.
 
Imetutoa kwenye uchumi wa chini mpaka wa kati wa chini, Sasa funga mkanda maana nchi inakwenda kwenye uchumi wa kati wa juu. CCM chama bora kabisa, Magufuli Rais bora kabisa. Tanzania nchi bora kabisa.
Yaani mnashindana kwa uwongo wakubwa na wadogo nyote mpo sawa,tatizo mnadanganyana wenyewe kwa wenyewe sasa,

Yaani mnajipa moyo kama yule waziri wa Iraq Tariq Aziz.bado mna tamaa mnashinda
 
Mimi sina chama ila naona CCM na Magufuli wanafanya kazi nzuri na wanapendwa sana
Kwangu mimi upo sahihi na ni haki yko kikatiba ila naomba tu ujifunze au uwafunze hao wanao pendwa kuvumilia na kuheshim mawazo ya wengine hii nchi yetu sote sio shamba la mtu yyote..
 
CCM akili zimesha ganda, hao polisi ni watoto wetu,ndugu zetu,baba zetu,mama zetu hata wao wanaishi kwa shida ''The truth will prevail'
 
Kule CCM ilikotutoa ndiko inakotupeleka.
 
Mimi sina chama ila naona CCM na Magufuli wanafanya kazi nzuri na wanapendwa sana
Kumbe bwana jela naye ni kipofu!!!,,,
Sasa wafungwa wote si watakutoroka wakuache hapo peke yako mkuu wangu??!!
 
Imetutoa kwenye uchumi wa chini mpaka wa kati wa chini, Sasa funga mkanda maana nchi inakwenda kwenye uchumi wa kati wa juu. CCM chama bora kabisa, Magufuli Rais bora kabisa. Tanzania nchi bora kabisa.
Anayeelewa ID yako inamanisha nini hawezi kukushangaa ukiandika hivi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…