Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,335
- 72,800
Hali sio shwari ndani ya serikali ya CCM na ndani ya Chama ila watu wanajitia upofu na kuona kila kitu ni kawaida tuu.
Matamko ya siku za karibuni kwa baadhi ya mawaziri kama Nape, Mwigulu na Majaliwa pia ukimya kabisa wa watu kama Makamba na mawaziri wengine ni dalili za kuonyesha kuwa kuna kuziriana kazi au kuamua kuwa "watajijua"
Kwenye Chama Mzee Mangula na Katibu Mkuu Kinana ndio kama wako sabbatical leave huku kijana Polepole akiwa amefunga breki ile speed yake aliyokuja nayo baada ya kuona mambo sio.
Lingine lenye utata ni kwa Wabunge wa CCM kujiweka karibu sana na viongozi wa upinzani jamba ambalo hapo awali halikuwepo na kwa mara ya kwanza imeonekana Bungeni hoja ya mbunge wa Upinzani ya kutaka Viongozi wa serikali ya CCM waitwe Bungeni ili waadhibiwe iki ungwa mkono na wabunge wote wa CCM wakiwepo mawaziri.
Siasa ni ushawishi na Mwnyekiti wa CCM anajisahau na kutumia mkono wa chuma wa serikali ndani ya chama badala ya ushawishi. Jee wazee wa CCM na waasisi wake wamekubali chama chao wakione kinajifia kwa kasi kama hii au watachukua hatua kwa kumuadhibu mwenyekiti wao? Ikumbukwe kwa katiba ya CCM vikao vya juu vya Chama vinao uwezo wa kumpigia kura ya kumtoa madarakani mwenyekiti tena krahisi kabisa.