CCM inakaribia kufa?

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,842
Reaction score
31,073
Msingi Mkubwa wa Chama chochote cha siasa kwenye ushindani wa vyama vingi, ni namna kinavyoweza kujenga hoja dhidi ya hoja zinazoibuiwa na upinzani, na hatimaye wananchi waweze kubaini kuwa walichoaminishwa na upinzani kumbe ni " fix" tupu!

Tokea serikali ya awamu ya 5 ya Chama kikongwe CCM iingie madarakani miaka takribani 2 iliyopita, wao wamekuwa na kazi moja ya kupambana na wapinzani huku wakiwa "assisted" na Jeshi la Polisi kuhakikisha kuwa vyama hivyo makini vya upinzani vinakufa!

Mbinu nyingine wanayotumia hao CCM ni kuwanunua wapinzani kwa fedha taslimu au kuwaahidi vyeo, wakiamini pia kuwa kwa njia hizo wataua upinzani nchini.

Nipende kuwaambia hao maccm wanaoamini kuwa wataua upinzani kwa njia hiyo kuwa wanajidanganya kupita kiasi, kwa kuwa wanazidi kuviimarisha vyama hivyo kwa kuwa wananchi walio wengi hivi sasa wamebaini mbinu hiyo ovu ya CCM na hivyo kuwajengea chuki zaidi chama hicho kikongwe kabisa hapa nchini.

Niwaambie CCM kuwa warudi kwenye misingi iliyokianzisha chama hicho ya kurejea kuimarisha idara ya uenezi wa Chama, katika kujibu makombora ya upinzani, na kamwe wasidhani kuwa kwa kutumia "pyupyu" ndiyo wataua upinzani.

Upinzani hapa nchini hautauwawa kwa mitutu ya bunduki na wala kwa kuwanunua wapinzani, watu waachiwe waone juhudi za maendeleo zinazofanywa na serikali yao ya CCM na hapo ndipo kwa hiyari yao kila mtanzania ataona umuhimu wa kujiunga na CCM.

Na kama CCM wataendelea na mtindo wao waliounzisha wa kutumia Jeshi la Polisi kuwatisha wananchi wasio na hatia na kuwabambikia kesi, hakika tutazihesabu siku za chama cha CCM kuendelea kubaki madarakani.

Na hakika zipo kila dalili za the last minutes of the dyeing horse.......

Kwa maneno mengine ni kuwa VERY SOON, CCM watalazimika kuachia madaraka, kama watapuuza ushauri huo muhimu wa wao kuendelea kusurvive.

Mungu ibariki Tanzania na uwabariki wananchi wake wabaini Sera nzuri wanazohubiriwa na wanasiasa, whether ni kutoka chama tawala au kutoka upinzani.
 
Kwenye siasa ni lazima itumike principle ya kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza.......

Ukiona kwenye siasa unatumia principle ya kumnyamaziisha mpinzani kwa "pyupyu" ujue chama hicho kinaelekea kaburini!
 
Ni ukweli ulio wazi sisiem ishakufa kwa sasa imeshikiliwa na vyombo vya dora,,,vyombo vya dora ndio vinashindana na vyama vya upinzani
 
hahaaaa na pia ukiona chama chako hakina sera ila kinajua maana tu ya dikteta uchwara ...na kirefu cha jpm..na kutafsiri sehemu ya maneno ya hotuba ya mkuu....kimbia mapema
 
kiongozi umenena,ccm inaanza kufa kwani kitendo cha kuwatoa nje mawakala wa upinzani ili kujifanyia uchaguzi haramu hata uingereza ilifanya kule zanzibar 1953,Makaburu walifanya Afrika kusini,Zambia ,Zimbambwe nk lakini ikafika mwisho,Nani hamfahamu mugabe yuko wapi?
 
kile kipigo cha tarehe 26 kimewachanganya akili pamoja na kupigwa 42 kwa moja bado unajiona we ndo mshindi kweli nyumbu mpo katika ubora wenu
 
Ni kweli CCM inaweza ikafa lakini kutokana na wapinzani kuwa usingizini wakati wa mazishi ya CCM basi itawafanya watanzania waendelee kulala wakiomba juu ya kaburi la CCM mana hawajui kuwa kuna mrithi wa marehemu.
Wapinzani wamebweteka hawaoni kuwa wana nafasi ya kupenya katikati ya mipango mibovu ya CCM kisiasa ,kiuchumi na kijamii.

KISIASA:
CCM wameanza kutuletea siasa za chuki na kukatana mapanga na kijenga roho chafu za kutojali maisha ya watu wengine zaidi ya madaraka.
Hili kwa wenye akili nje ya madaraka wanalichukia na kulilaani sana.Kwa wenye madaraka ndani ya CCM na serikalini kwao hii ni mbinu ya kukalia madaraka bila kupingwa au kukosolewa au kubughudhiwa . Uhuru wa watawala kutawala kwa mabavu.

KIUCHUMI:
CCM wameturudisha kwenye kauli ya maskini Jeuri.
Huku watawala wakiwa matajiri wasio na njaa lakini wanakua wajeuri kusikiliza kilio cha maskini.
Mipango hafifu ya ndani na nje ya serikali ya CCM ni kikwazo cha kukua kwa uchumi wa wananchi zaidi ya serikali kukomba pesa za wananchi kupitia kodi kubwa na riba kubwa za mabenki kwenye vibiashara vile vile vilivyokuwepo kwenye wakati ulippita bila kuwa na mbinu mpya za kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja.

KIJAMII:
CCM na serikal yake wameyumba sana kusimamia haki,usawa, uhuru,utu,umoja wa watanzania ,upendo miongoni mwetu na hata ule utani wa makabila huko tunakoelekea utapotea mana kuna watu wanachukiana wazi wazi kutokana na makabila na kanda zao lakini hatuoni juhudi za kuwaleta watu pamoja tangu uchaguzi mkuu ulipopita 2015 .
Kwa mara ya kwanza tunaona siasa zikitawaliwa na shutuma za ukabila.
Wasanii wamegeuka kuwa makada wa CCM kutokana na kuhofia hatma ya kazi zao.
Sana zimedoda kutokana na jamii kugawanyika.
Ni wazi kuwa vijana wengi ni Chadema na CUF na sasa ACT wazalendo ; sasa msanii anapojitangaza kuwa mwanaCCM anapoteza mvuto ghafla kwa vijana ambao wengi ni wapinzani.
Hapo ni lazima msanii huyo apambane na hali yake akiwa ndani ya CCM na kujitafutia fursa zingine ndani ya CCM kwa kuwa mitaani anakosa mvuto.


Niwakumbushe tu CCM kuwa kuna umuhimu mkubwa sana kwa nchi yetu kuwa na mfumo imara wa vyama vingi kutokana na kuongeza upana wa uwanja wa kisiasa.
Ukifukuzwa CCM unakimbilia upinzani. Ukifukuzwa upinzani unakimbilia CCM.

Kuna wakati mtu anakerwa na mambo ndani ya chama hivyo anapata nafasi nyingine upinzani.

Sio kila anayehama kwenye chama ana makosa.
Mwingine anahama kwa kukerwa na mambo ya dhulma na mwingine kwa kuona kuwa chama hakina nia na uwezo wa kuingia madarakani au kutoa afasi za madaraka. Kila mtu ana sababu zake.
Mwisho wa yote nafasi zitajaa na dhulma hazita isha kamwe. Ndio maana hata huko Denmark kuna vyama vya upinzani na wanaharakati wa kutetea haki za binadamu.
Binadamu alianza kutetewa enzi na enzi.
Zama hizo watetezi wa haki za binadamu waliitwa Manabii na Mitume. Hao walitetea haki na usawa mpaka kufa. Waliishi maisha ya umaskini lakini hawakujali .Walitishwa lakini hawakukata tamaa. Hawakuhongeka wala kuhama na kufuata nia za watawala.


CCM INAELEKEA KUFA LAKINI MRITHI WAKE MPAKA SASA HAJITAMBUI NA YUKO MBALI NA FAMILIA.
 
Watz hawako tayari kuwapa nchi.Heri matatizo ya CCM kuliko shida tukazoenda kuzipata dhidi ya walaghai wa CDM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…