Maisha yanaenda yakibadilika kila siku,tekinoloji nayo inabadilika na hata uwezo wa watu wa kutazama mambo unabadilika.
Katika chaguzi zilizopita CCM haikuwa na kazi kubwa sana.Watu ambao hata bila kufanyiwa kampeni waliipigia kura CCM walikuwa wengi.Upinzani ulikuwa umegawanyika na haukuwa na wafuasi wengi sana.Ilikuwa rahisi sana kwa CCM kuhujumu,kudhulumu na kushinda hata kwa single moja tu ya kapteni Komba.
Jambo ambalo CCM hawajaweza kulimeng'enya ni kwanza kutambua athari ya muungano wa vyama vya upinzani na Pili athari ya Vigogo waliokuwa CCM waliohamia upinzani.
Mambo haya mawili yamebadili upepo katika uwanja wa kampeni na CCM ilipaswa kutambua hili.
Kwanza Muunganiko wa Upinzani umewafanya wafuasi wa upinzani kuwa kitu kimoja na kuzungumza lugha moja na hili limeongeza mara dufu wapiga kura wa mgombea wa upinzani wenye maamuzi tayari~decided voters.
Pili kuhamia upinzani kwa waliokuwa vigogo wa CCM kumeimega CCM kwa sehemu kubwa na waliomegeka ni wapiga kura wenye maamuzi tayari.
Ni kukosa kufikiri tu kutamfanya mgombea yoyote kati ya Lowasa na Magufuli wajinadi kwa wafuasi wachache ambao kimsingi ni wafia chama wa Act na TLP.
Kwenye kampeni za kisasa,vyama na wagombea huweka mikakati mingi juu ya wapigakura ambao hawajafanya maamuzi~undecided voters.
Swali linakuja,Wapiga kura ambao hawajafanya maamuzi ni wapi katika uchaguzi huu?
Jibu liko dhahiri; ni wanachama waliobakia CCM na wapiga kura wachache wasio na vyama.
Kampeni za toroka uje,vuka mto,ulipo tupo zinawalenga wapigakura waliobakia CCM.
Sera za elimu bure,riba kwa mkulima na nyingine zinawalenga wapigakura wasio na vyama zaidi!
Hii inaitwa "targeting in campaign".
CCM inauza sera za jumla jumla kwa watu wote.Unaweza kurusha jiwe kwenye kundi la ndege elfu usipate hata mmoja.
CCM haijui wafuasi wake kindakindaki wamebaki wangapi na wala imlenge nani,hii ni hatari kubwa.
Kampeni za tshirt,wali na kofia ni kampeni za kizamani.
Kampeni za kisasa ndio hazina ilani, eti!
Mfanyabiashara kama mbowe na mwenzie lowassa wamesha fanya biashara nyingi sana tangu ujana wao haswa mbowe na mali zake za kurithi hao watu kili kitu kwao ni dili kama ww unapoletewa dili hata la vitu vya wizi na unalikurupikia tu ki mtaani mtaani! Katika dili za kiujanja ujanja mbowe kesha uza chama hiyo kwake ni top deal kachukua vyake sshv anasikilizia kuuza nchi na jiiizi la kimataifa! Kama huyo mwingine ana mali na biashara zake nzuri tu mbali na wizi bado angeendelea kuishi vzr ila sijui kwann watu wa aina hii hawaridhikagi! Na katika dili hili wakiliweza wao ni ma expert wa kimataifa!Ndugu yangu,fungua macho uangalie,kampeni za CCM zimeanza kama mtu anayeendesha gari usiku bila taa,huwaga hawezi ona hatari iliyo mbele kwa muda sahihi.
Kwanza tu,Magufuli anakosa sifa ya kiuongozi ya kushawishi mabadiliko,sasa hivi watu wana kiu ya kiongozi anayeweza kutingisha taasisi na magufuli hanukii wala harufu hiyo.
Alafu tuseme tu kweli,Kikwete aliboronga na hii inamfanya asiwe mtu sahihi wa kumnadi Magufuli kwenye majukwaa.Anabana wigo wa kura.Brother toroka uje,better late than never.
Magufuli na Kikwete,tuseme CCM kwa kifupi kutumia ujenzi wa barabara kutafutia kura ni sehemu ya uelewa mdogo.
Wakati ni kweli kwamba barabara ni jambo la msingi sana lakini kura kwanza hazitolewagi kama pongezi au zawadi,pili hamna kundi katika jamii linalofaidika lenyewe tu binafsi na barabara.Hapa naomba nieleweke vizuri,wanafunzi pamoja kuwa wananufaika na barabara lakini wanajali zaidi gharama za elimu,ubora wa elimu na ajira.
Wafanyabiashara pamoja na kuwa wanafaidika na barabara wanajali zaidi kodi,upatikanaji wa mikopo na unafuu wa huduma za fedha.
Vivyo hivyo kwa makundi mengine.Barabara ni hoja ya ujumla sana,think tank ya kampeni ya CCM inapaswa kufikiri zaidi.
Kabisa walishaambiwa watafute namna ya kukutana na makundi mbali mbali na kuongea nao wao wanawaita mmoja ya wawakalishi wao katika kadamnasi za jumla aongelee faida za sera za CCM.Magufuli na Kikwete,tuseme CCM kwa kifupi kutumia ujenzi wa barabara kutafutia kura ni sehemu ya uelewa mdogo.
Wakati ni kweli kwamba barabara ni jambo la msingi sana lakini kura kwanza hazitolewagi kama pongezi au zawadi,pili hamna kundi katika jamii linalofaidika lenyewe tu binafsi na barabara.Hapa naomba nieleweke vizuri,wanafunzi pamoja kuwa wananufaika na barabara lakini wanajali zaidi gharama za elimu,ubora wa elimu na ajira.
Wafanyabiashara pamoja na kuwa wanafaidika na barabara wanajali zaidi kodi,upatikanaji wa mikopo na unafuu wa huduma za fedha.
Vivyo hivyo kwa makundi mengine.Barabara ni hoja ya ujumla sana,think tank ya kampeni ya CCM inapaswa kufikiri zaidi.
Mleta mada una akili sana. Umeandika vitu vya msingi sana, CCM wanafanya vitu kwa mazoea wakidhani watanzania watawachagua tu, kumbe hali sio shwari.
Tayari Magufuli amefanya kampeni katika mikoa 6(Dar, Katavi, Rukwa, Mbeya, Njombe na sasa yuko Songea) lakini Political atmosphere inamtisha sana Magufuli, hali ni tata sana.
Mood iliyopo kwa watu wanaohudhuria mikutano yake haitoi matumaini ya Ushindi kwa CCM hata kidogo, bahati mbaya Viongozi wa CCM hataki kukubali huu ukweli.
Nadhani Think tankers wa CCM na Magufuli ama ni wazee sana kisiasa(wamechoka), mambumbu wa siasa za kisasa au wamebweteka kama sio kukata tamaa.