CCM ina agenda gani na viongozi wa jeshi?

Mapambano Yetu

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2012
Posts
1,133
Reaction score
2,128
Nimekuwa nikifatilia Wakuu wa Majeshi hasa jeshi la wananchi pale wanapostaafu, kilichonifanya kuleta mada hii ni baada ya kutafakari na kuona kuwa yawezekana kuna agenda ya siri kati ya CCM na viongozi wa ngazi za juu jeshini. Viongozi wa Jeshi wamekuwa wakitunukiwa vyeo serikalini hasa Ukuu wa wilaya au Mkoa.

Kwa kufanya hivi nahisi inaweza kuwa mbinu inayotumiwa na CCM ili viongozi wote jeshini wawe upande wao kwa lengo la kutunukiwa u DC pale watakapostaafu. Kwa uelewa wangu mdogo GENERALI huendelea kulipwa mshahara hata baada ya kustaafu.

Kutokana na hilo kuna umuhimu gani wa kumteua mtu kama huyu kuwa Mkuu wa Mkoa? Je, huku sio kujipendekeza kwa vingozi wengine ambao hawajastaafu ili wawe upande wao na kutetea maovu yao? Ukilinganisha hili na tukio la kiongozi mmoja wa jeshi ambaye aliwahi kutumiwa kutoa vitisho kwa viongozi wa upinzani wakati wa uchaguzi mkuu wa2010 utatambua fika kuwa yawezekana kuna mpango wa siri kati ya CCM na VIONGOZI wa jeshi.

Naomba kuwasilisha.
 
"Nakusamehe kwa kuwa umekili uelewa wako ni mdogo" Kwa faida ya wengine ni Kwamba General Baada ya kustaafu haendelei kulipwa mshahara bali mafao yake ya uezeeni kwa kutambua utumishi wake kwa kulitumikia taifa.
 
Uko sahihi kabisa. Hii ni kete ambayo ccm huwa wanaitumia kila wakati ili kuwarubuni maafisa wa jeshi wawe upande wao.
 
Jeshi lipo kwa maslahi ya TAIFA. MaCcm Yasitegemee kuwa JESHI kwa sasa linawaangalia wao, kiukweli WANAJESHI wengi Mioyo yao Ipo CHADEMA. Hongereni WANAJESHI wanaoi'support CHADEMA kwa kila Namna. Najua MNAJIJUA na Wengine Tuko pamoja. SALUTI.
 
"Nakusamehe kwa kuwa umekili uelewa wako ni mdogo" Kwa faida ya wengine ni Kwamba General Baada ya kustaafu haendelei kulipwa mshahara bali mafao yake ya uezeeni kwa kutambua utumishi wake kwa kulitumikia taifa.
Nashukuru kwa msamaha na masahihisho yako. lakini message bado ni ile ile, huoni kuwa kuendelea kuwapromot watu hawa ni njia majawapo ya kutongozea urafiki baina ya CCM na Maofisa wa Jeshi? Je haki itaweza kutendeka kwa misingi hiyo?
 
"Nakusamehe kwa kuwa umekili uelewa wako ni mdogo" Kwa faida ya wengine ni Kwamba General Baada ya kustaafu haendelei kulipwa mshahara bali mafao yake ya uezeeni kwa kutambua utumishi wake kwa kulitumikia taifa.

Hayo hayo mafao ndio kama mshahara ni lugha tu
 
Back
Top Bottom