ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 620
- 1,543
CCM IMEWEKWA MFUKONI NA SERIKALI
"Ndugu Polepole na viongozi kadhaa wa Serikali wamekaririwa wakisema kwamba vyama vya upinzani vinayatumia matatizo ya wananchi kama mtaji wa kisiasa. Bila shaka CCM imekwishazisahau nasaha za Mwalimu Nyerere. Mwaka 1968 Mwalimu Nyerere alialikwa na Chama cha UPC cha Uganda. Kwenye hotuba yake (Iliyoitwa THE PARTY MUST SPEAK FOR THE PEOPLE yaani “Chama lazima kiwasemee Watu”) Mwalimu anaweka bayana kuwa jukumu la Chama cha siasa ni kujishughulisha na matatizo ya watu. Mwalimu anaongeza, “Kwa kweli, serikali ndicho chombo cha chama na wala si chama kuwa chombo cha serikali”. Kwa jinsi mambo yanavyokwenda hivi sasa ni dhahiri kuwa CCM imewekwa mfukoni na Serikali na imeacha jukumu lake la kuisimamia serikali na kuwatetea wanyonge. Ingekuwa inautambua wajibu wa vyama vya siasa kama ulivyopambanuliwa na Mwl Nyerere, CCM isingewashangaa wapinzani kuwasemea watu kwa sababu huo ndio hasa wajibu na ‘’mtaji halali” wa Chama chochote cha siasa.
Ndugu Ado Shaibu,
Mazungumzo na Waandishi wa Habari,
18/01/2017