mr mkiki
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 5,722
- 11,930
Nitahitimisha mjadala huu kwa kuchambua makundi mawili yaliyopoteza fursa ya kumshauri rais wenu.
Kundi la kwanza la washauri rasmi wa rais ni baraza la mawaziri. Hiki ni chombo muhimu sana chenye hadhi ya juu ya kumshauri rais. Ni vema kueleweka kwamba baraza la mawaziri ni tanuru la fikra la rais.
Ndio maana katika baadhi ya nchi zenye mifumo dhabiti ya kitaasisi waziri mara baada ya kuteuliwa hutakiwa kudhibitishwa na mamlaka nyingine.Lengo ni kwamba mtu anayetakiwa kumshauri rais anapaswa kuwa mtu makini,mweledi na mwaadilifu. Mara nyingi bunge hutumika kama sehemu ya kuidhinisha wateule wa rais.
Bunge ni eneo nyeti lenye utakatifu na upekee wa aina yake. Viongozi wakubwa wa dunia,wafalme na wenye mamlaka hawapendi hata kutembelea maeneo ya bunge. Katika nchi zinazoheshimu demokrasia, Bunge lina heshima kubwa kuliko hata mhimili wa utawala na ule wa mahakama
Kwa sababu ndipo sheria hutungwa na ndipo viongozi wa mhimili wa utawala huidhinishwa, wakiwemo mawaziri na wateule wengeni wa mhimili wa utawala, Kwa hiyo,baraza la mawaziri ndipo chombo cha juu cha ushauri kwa taasisi ya urais.
Kuthibitisha hoja hiyo, Katiba ya jamhuri ya muungano ya mwaka 77 ibara 54(3) inasema "bila ya kuathiri masharti yaliyomo Katika ibara ya 37(1) ya katiba hii, Baraza LA mawaziri litakuwa ndicho chombo kikuu cha kumshauri raisi juu ya mambo yote yanayohusika na utekelezaji wa madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya katiba hii,na litamsaidia na kumshauri rais juu jambo lolote litakalowasilishwa kwenye baraza hilo kwa mujibu wa maagizo maalum au maagizo ya jumla yatakayotolewa na rais
Pamoja na ukweli huu, rais halazimishwi kufuta ushauri wa mtu yoyote. Anaweza kusikiliza ushauri, lakini asiufute. Anaweza akajigeuza mshauri mkuu wa kushauri washauri wake mwenyewe.
Mlolongo huo mrefu unaweza kutengeneza ugumu wa kumshauri rais, Kwan hofu kwamba, si lazima ushauri ufuate. Huu umekuwa mlima mwingine mrefu Sana kwa washauri hawa rasmi kuukwea. Wengi huchagua kukaa kimya kwa kuhofia kuwa wanaweza kueleweka vibaya ama wasaliti wa dhamira ya rais. Mara nyingi, viongozi wengi wa kiafrika hupenda sana kushauriwa yale wanayojishauri wenyewe wakiwa faragha!
Kundi la pili la washauri wa rasmi wa rais ni chama cha rais ambacho kinaingia moja kwa moja kwenye kundi rasmi la kumahauri. Sababu zipo mbili: mosi chama ndicho chenye ilani inayotekelezwa na serikali iliyopo madarakani.
Mifumo yetu ya uchaguzi inatoa fursa hiyo, yaani chama kinachoshinda kinachukua Lila kitu "winner take all". Katika msingi huohuo, CCM wanna turufu ya kumshauri rais, fursa wanayoanza kuipoteza sasa.
Pili, udhaifu wa serikali ni kushindwa kwa CCM. Chama cha mapinduzi Kama ilivyo kwa vyama vyote dola ndicho kilichoingia mkataba na wananchi.
Mkataba huu ni miaka mitano na mtekelezaji ni serikali.
Ni bahati mbaya Sana, CCM imepoteza fursa hiyo ya kitaasisi katika kuishauri serikali.
Sent using Jamii Forums mobile app