sir.JAPHET
JF-Expert Member
- May 18, 2012
- 699
- 137
Dalili mojawapo kubwa ya ulevi hasa wa pombe ni kutumia pombe kama mwarobaini. Yaani pombe inakuwa ni dawa ya kutibu kila kitu, mtu akifiwa analewa, akifurahi analewa, akichoka analewa, akisafiri analewa, akiwa na sherehe analewa, akikasirika analewa, hivi pombe inakuwa jawabu la kila kitu. Basi huyu anakuwa tegemezi kwa pombe hivi anakuwa amepoteza uwezo wa kufanya chochote bila kulewa pombe.
Chama kikifikia hapa basi badala ya kutumia elimu na taaluma za watu kinachotumika ni propaganda za siasa kutatua matatizo na kero za wananchi. Kwa mtindo huu hatuwezi kupata maendeleo kwa sababu siasa inakuwa ni kila kitu, mfano kutatua matatizo ya walimu unaweka siasa, mgogoro wa madaraka weka siasa, kuelezea kifo cha mwandishi wa habari kama kile cha Daudi Mwangosi inaingia siasa. Siasa inakuwa ni kama mwarobaini wa kutibu magonjwa yote. Ndiyo kwa maana nasisitiza kwamba CCM imelewa madaraka inapaswa kutibiwa ugonjwa huu wa ulevi wa madaraka.
Katika hatua hii mlevi anakuwa amechanganyikiwa, hajitambui ana black out. Ulevi wa CCM umefika hapo ambapo viongozi wake wengi hawakumbuki sasa misingi mizuri ya CCM ya usawa, haki, utu, amani, utumishi na kujali wananchi wake ambao walikuwa ndiyo wenye chama yaani wa kulima na wafanyakazi.
Chama kilikuwa mali ya wananchi na si vigogo na hasa mafisadi. Hapo ndipo tunapoona kweli chama tawala kimelewa madaraka na kimepoteza muelekeo ule alioutabiri hayati Horace Kolimba Katibu wa kwanza wa CCM. Kwa mtindo huu tunapata wapi ujasiri wa kusema kwamba hii ndiyo CCM ya Nyerere? CCM ya Nyerere haikuwa ya matajiri na mafisadi, bali ya wananchi yaani wakulima na wafanyakazi. CCM ya Nyerere iliheshimu na kukuza Azimio la Arusha, lakini leo tunakuza Azimio la Rushwa.
CCM ya Nyerere iliwaheshimu wananchi bila ubaguzi, lakini sasa wanaosikilizwa ni matajiri, vigogo na mafisadi. CCM ya Nyerere haikuwa na udini, leo udini unaingizwa katika kampeni za kuchagua viongozi wa taifa ona jinsi CCM ilivyotumia udini Igunga na Arumeru. Hii ni propaganda ya CCM ni lazima tuikatae ama sivyo makanisa na misikiti itakuwa mahali pa kutoleana matusi na kashfa.
CCM ya Nyerere haikutumia matusi ya nguoni kama ilivyofanyika katika kampeni za kisiasa huko Arumeru. CCM ya Nyerere ilikuwa hainunui uongozi kwa rushwa, ilikuwa haitumii polisi kutishia wananchi katika chaguzi mbali mbali. CCM ya Nyerere ilikuwa haitumii pesa ovyo kupeleka maji yanayowasha katika maeneo ya kupigia kura kwa nia yakuwanyanyasa na kuwatishia wapiga kura. CCM ya Nyerere haikujigamba itatawala milele, kwa sababu alijua anayetawala milele ni Mungu peke yake.
CCM ya Nyerere iliunganisha wananchi bila kujali cheo, kabila, rangi, utajiri, dini au maskini wote walikuwa kitu kimoja. CCM ya leo imeleta ubaguzi wa kikanda, dini, makabila, matajiri na maskini na kadhalika.
Matokeo yake CCM ya leo imekuwa kama mnara wa Babel, jamii ambayo ilikuwa inajigamba kwamba itajenga mnara wa kuweza kumchungulia Mungu. Matokeo yake Mungu aliwasambaratisha kwa sababu ya majivuno yao.
Leo ninaposikia baadhi ya viongozi wakijigamba kwamba CCM itatawala milele, mimi napiga kifua changu na kusali Ee Mungu uturehemu, kwa maana anayetawala milele na enzi ni yake ni Mungu pekee yake. Je, hii si kufuru katika medani hizi za demokrasia ya vyama vingi? Je, ukomavu wa demokrasia ndani ya vyama vingi upo wapi? Tukubali kwamba Tanzania bado changa katika siasa za vyama vingi, mbona vurugu, maasi na vifo vingi katika mikutano ya kisiasa na nani anawajibika, ni wale wenye serikali kulinda raia na mali zao.
Nia ya chama tawala na vyama vingine vya kisiasa sasa ni kutaka kubaki ikulu kwa gharama zozote zile. Ukisha uchaguzi mara ni kuanza kampeni za uchaguzi mwigine, je, ahadi mlizotoa mtazitimiza saa ngapi? Tunataka maendeleo ya wananchi na si maendeleo ya kisiasa, ya vyama, wala ya watu kubaki katika madaraka yao. Tunataka maendeleo katika elimu, afya, miundo mbinu (barabara, umeme, maji safi, kilimo, utamaduni na maendeleo ya watu si vitu kama alivyosema Baba wa Taifa katika kitabu chake cha Binadamu na Maendeleo.
Ni kweli Watanzania wenye macho ya kuona vizuri nini kinaendelea katika nchi yao wanaona wazi CCM imelewa madaraka. Imelewa madaraka ya kisiasa, yaani imelewa siasa kwa maana kwamba siasa ni tiba ya kila kitu. Migomo ikitokea vyuoni tiba yake ni propaganda za kisiasa, madaktari wakigoma Muhimbili tiba yake ni siasa, wafanyakazi wanadai haki zao tiba ni siasa, umeme usipopatikana tiba yake ni siasa, ajali zikipatikana tiba yake ni siasa na mauaji yakitokea katika mikutano tiba yake ni siasa.
Ukiulizia ipi ndiyo sera ya nchi yetu sasa, ni ujamaa na kujitegemea au ubepari hakuna jibu sahihi linatolewa. Je, sera ya madini yetu yanayotajirisha wageni ipi ? Na ukiuliza hata kiongozi mkuu wa nchi kwa nini nchi ni maskini, naye anasema hata yeye hajui, je, huku si kukosa mwelekeo? Taifa letu limetumbukia mahali pabaya, wananchi wengi wanajua hilo hasa vijana na wasomi wa vijijini na mijini.
Vijana hawa ndio sasa wanadai mabadiliko ya kisiasa, ya kiuongozi, na kiuchumi. Wananchi wamechoshwa na sera mbovu za kilevi za CCM.
Dawa pekee ni kuipumzisha CCM kwa kutumia sanduku la kura mwaka 2015 ili ikatibiwe, kikiwa chama cha upinzani kama inataka kuendelea kupumua na kuishi. Watanzania tuungane tuikomboe nchi yetu kutoka katika utumwa wa mawazo, demokrasia, utawala bora na uporaji wa rasilimali zetu.
Nchi hii inahitaji hatua nyingine ya ukombozi.
Njia mojawapo nzuri ni kupata Katiba mpya kama sheria mama yenye kuainisha tume huru ya uchaguzi, madaraka ya rais, rushwa katika chaguzi, matumizi ya uwazi ya daftari la wapiga kura na mambo mengine nyeti kama matumizi ya vyombo vya dola, vyombo vya habari vya taifa, tunaweza kufanya hilo tukizingatia mafundisho ya Baba wa Taifa aliyowahi kusema: Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.