''CCM imekufa na sasa inajizika yenyewe''

Concrete

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2011
Posts
3,605
Reaction score
551
Hayo ni maneno machungu sana kwa mwanaCCM yoyote lakini ndio niliyoyasikia kutoka kwa kada mmoja mwandamizi wa CCM akiyasema kwa uchungu sana.

Alifafanua kwa kusema Chama ni WATU(Quality na Quantity), ITIKADI(Principle na Philosophy) na SERA(Vision na Mission). Kwa sasa CCM tuna watu wachache na hafifu sana kisiasa, hatuna itikadi yoyote( maana ujamaa tulishauzika kimya kimya) na miiko na maadili tulishayaacha(tuna-survive kwa fitna, Rushwa na ufisadi), Sera zetu hazina msaada wowote kwa mnyonge, maskini, mkulima au mfanyakazi. Tumebaki kuigaiga mambo ya wapinzani wetu na kupambana nao utadhani wao ndio chama tawala.

*MY TAKE
WanaCCM wenye uchungu na nchi yetu na chama chetu tunajifunza nini katika hili lakini wapinzani wetu mnalichukuliaje hili?
 
Hivi vyama vyetu vilivyopigania uhuru vina matatizo yanayofanana....vilidhani vina hatimiliki ya kushika na kutawala dola.
Maonyo na ushauri mwingi ambao CCM walipewa kwa miaka mingi tu haukuzingatiwa bali kupuuzwa. Mwishowe wanakuja na vitimbi, vitisho na mauaji.

Wafe salama na haraka tu, wametuharibia hii nchi na kuidumaza.
 
Tatizo lao ni kujiamini bila kujua hata wapinzani walikuwa chama hicho hicho.
 
Fitina, uongo na vitisho ndio sera ya ccm, zaidi ya hapo ni mbinu za kuua vyama pinzani wakati awaangalii sababu zinazowafanya ccm iwe ICU.
 
Ukitaka uwe na uhakika kabisa kuwa CCM haipo mioyoni mwa waTanzania.....jikumbushe kipindi cha asubuhi njema leo Channel ten, miaka 36 ya Uhuru ..alikuwa anahojiwa Mwingulu, katika simu zote zilizopigwa kama nane hivi...zote wapiga simu wote waliiponda CCM, ilikuwa aibu!!!
 
Hayo ni maneno machungu sana kwa mwanaCCM yoyote lakini ndio niliyoyasikia kutoka kwa kada mmoja mwandamizi wa CCM akiyasema kwa uchungu sana.

Alifafanua kwa kusema Chama ni WATU(Quality na Quantity), ITIKADI(Principle na Philosophy) na SERA(Vision na Mission). Kwa sasa CCM tuna watu wachache na hafifu sana kisiasa, hatuna itikadi yoyote( maana ujamaa tulishauzika kimya kimya) na miiko na maadili tulishayaacha(tuna-survive kwa fitna, Rushwa na ufisadi), Sera zetu hazina msaada wowote kwa mnyonge, maskini, mkulima au mfanyakazi. Tumebaki kuigaiga mambo ya wapinzani wetu na kupambana nao utadhani wao ndio chama tawala.

*MY TAKE
WanaCCM wenye uchungu na nchi yetu na chama chetu tunajifunza nini katika hili lakini wapinzani wetu mnalichukuliaje hili?

Ukitaka uwe na uhakika kabisa kuwa CCM haipo mioyoni mwa waTanzania.....jikumbushe kipindi cha asubuhi njema leo Channel ten, miaka 36 ya Uhuru ..alikuwa anahojiwa Mwingulu, katika simu zote zilizopigwa kama nane hivi...zote wapiga simu wote waliiponda CCM, ilikuwa aibu!!!
 
TUNASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MAREHEMU CCM. WASIFU WA MAREHEMU:
Marehemu alizaliwa 05/02/77.
Atazikwa 25/10/2015.

Enzi za uhai wake marehemu alijishu ghulisha na kuua mazao ya biashara: Kama vile pamba, tumbaku, kahawa, korosho, mkonge nk.
Marehem pia atakumbukwa kwa bidii ya kutaifisha na kuua viwanda & makampuni ya umma na vyama vya wakulima. Atakumbukwa kwa ufisadi na ubadhirifu wa fedha na kodi za umma.

Pia amewaleta na kuwapa wageni mali za wa TZ . Marehemu ameacha wachina kariakoo, waarabu Loliondo, makaburu mererani na wazungu wa kila aina kwenye migodi.
CHANZO CHA UMAUTI wake ni GESI YA MTWARA
 
Back
Top Bottom