CCM ‘IMEJIUA’, inasubiri kuzikwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM ‘IMEJIUA’, inasubiri kuzikwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mizambwa, Jun 13, 2012.

 1. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  CCM ‘imejiua’, inasubiri kuzikwa


  Bila kutafuta maneno, mgogoro ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) umekuzwa na kupata nguvu baada ya Jakaya Kikwete, kukubaliana na matakwa ya wachache ya kuvunja Kamati Kuu (CC) na sekretarieti yake iliyokuwa inaongozwa na Katibu mkuu wake, Yussuf Makamba. Hapo ndipo mpini ulipoanza kuungua.


  Ni tukio hilo lililoingiza sektarieti na kamati kuu iliyochoka. Ikaibuka na utafiti dhaifu uliozaa falsafa ya “kujivua gamba.” Hii ndiyo dhambi ambayo inaitafuna CCM mpaka sasa; hakuna njia nyingine mbadala ya kukiokoa chama hiki.


  Na John Kibaso, kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mbunge wa zamani wa Temeke.
  ...................................................................................................
   
 2. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Nakuwa tofauti kabisa na wanaosema CCM imekufa. Lugha hii imekuwa ikisikika sana tena kwa miaka kadhaa sasa. Mimi nitakachoweza kuamini ni kuwa CCM ni imara sana na ndiyo maana wapinzani wake wanatumia muda mwingi sana kukipaka matope, kuwalaghai wananchi na mambo mengine mengi ilimradi tu kionekane hakifai, lakini mara zote kimekuwa imara. Kama CCM kikngekuwa siyo imara kulikuwa hakuna haja ya kuhangaika huku na kule kukipaka matope na badala yake vyma hivi vya upinzani vingejikita kuwatatulia wananchi matatizo yanayowakabili. Hakika kitendo cha Vyama vya upinzani kuzunguka nchi nchi nzima kuwaeleza wananchi kuwa CCM ni mbovu ili hali wana macho na wanaweza kuona wenyewe ni dhahiri kuwa CCM kinaogopwa.
   
 3. B

  Babuu Rogger JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 80
  Nipo Musoma katika shule moja ya sekondari Mwisenge, nikamuona kijana mmoja mwenye umri wa miaka kumi na sita (kidato cha pili) ameshikilia kitambaa cha kujifutia jasho chenye rangi ya kijani, nilichofanya ni kamuita na kumpa vimaneno kidogo, nikamwambia "inaonekana wewe unaipenda sana CCM, kwa mshangao akaniuliza kwa nini!? nikamjibu kwamba kitambaa chake kina rangi ya kijani, akashangaa tena na kuniuliza swali, HIVI RANGI YA KIJANI NI YA CCM? nikamjibu ndio ni kijani na njano, pale pale yule kijana akakitupa kile kitambaa na kuniambia kuwa katika shule yao hakuna kijana atakaekipigia CCM kura katika uchaguzi ujao kwani wengi wao watakuwa wameshafikisha umri wa kupiga kura na wanaapa kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura" sasa hii ni shule moja Tanzania je zilizobakia zikoje kwani vijana wanaonesha chuki ya wazi kwa CCM hapo utasalimika kweli? imefikia vijana wanakwenda kucheza mechi za mpila wa miguu wanabeba bendera za CHADEMA na ukiwauliza kwa nini wanafanya hivyo wanasema wao ni peopleees. Sasa utakuja kusema CCM ina usalama. TAFAKARI. CCM haitashindwa kwa ajili ya migogoro yao VIJANA ndio wataomaliza mchezo.
   
 4. J

  JF-MBUNGE JF-Expert Member

  #4
  Jun 13, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 422
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Simple analysis...huyo Y.Makamba ndio aliyeanza kuiua CCM unakumbuka alivyokuwa anakashifu wana CCM wenzake hawana akili wanaokosoa mambo maovu kwenye chama?? secretariete mpya imekuta CCM mahututi tayari ...simple
   
 5. N

  Nteko Vano JF-Expert Member

  #5
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 436
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nembo yao inakiri hivyo. Jamaa alisema nyundo inatumika katika uchongaji wa jeneza na jembe kuchimbia kaburi
   
 6. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Ni ngumu sana kwa vyama vya upinzani kutatua matatizo ya Wananchi wa Tanzania; kwani hawana Dola, akaunti zote na Rasilimali za nchi zipo mikononi mwa Seikali ambayo inaongozwa na CCM.

  Leo ni ngumu kwa chama pinzania kujenga Barabara, Hospitali, Shule, nk.

  Hivi cyote vipo chini ya Serikali.

  MIZAMBWA
  NABII MTARAJIWA!!!
   
 7. N

  Nteko Vano JF-Expert Member

  #7
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 436
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Vyama vya upinzani vinajiimarisha vijijini sasa hivi ili kuleta upinzani wa kweli na hatimaye kushika dola na hili ndilo lengo la chama chochote. Kwa mfano CDM hakipaki matope bali kueleza ukweli juu ya utendaji mbovu wa serikali yetu. Kwani ni lipi linazungumzwa ambalo sio la kweli? Wananchi sasa hivi wameamka na wanatambua pumba ni zipi na wameonesha kuikubali CDM kwakuwa wameona yanayozungumzwa yana ukweli. Je, hakuna mfumuko wa bei? viongozi hawatumii madaraka yao kujinufaisha wenyewe? hakuna mikataba mibovu?. Wenyewe wameanza kukubali kwa mfano kauli za Membe, Masha na wimbi la wanachama wanaokikimbia.
   
 8. m

  mamajack JF-Expert Member

  #8
  Jun 13, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  utakuwa na mtindio wa ubongo wewe!!
   
 9. Badu

  Badu JF-Expert Member

  #9
  Jun 13, 2012
  Joined: Jun 2, 2012
  Messages: 363
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ra i p c c m
   
 10. Kalumbesa

  Kalumbesa JF-Expert Member

  #10
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,009
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ndugu yangu CCM ni merehemu tayari ni muda tu ndio unaozuia sisi kumzika leo. Mimi napoishi tunapakana na shule ya msingi jirani,mwalimu akifundisha watoto wa darasa la sita.."Daraja refu kuliko yote linapatikana nchini china na lina urefu wa kilomita 45. yaani ni kama hapa mpaka bagamoyo, au ni kama kuweka daraja feri mpaka zanzibar. Hata sisi tuna uwezo wa kujenga madaraja marefu na mazuri sema ndio hivyo hawa mafisadi wa CCM hawafai" si maneno yangu maneno ya mwalimu je watoto hawa wakikua utawaambia nini kuhusu CCM si wanaweza wakakuchimba kidevu
   
 11. f

  fered mbataa JF-Expert Member

  #11
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 19, 2012
  Messages: 240
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watatue matatizo wao ndo gvt? Hiyo shughuli ni ya ccm. Wapen dora wapinzani waondoe uccm muone maendeleo.
   
 12. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #12
  Jun 13, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,804
  Likes Received: 1,118
  Trophy Points: 280
  Ngoja nikumbuke kauli ya kiongozi wa zamani wa Ccm aliyewahi kusema Kikwete ni maarufu kuliko hata chama, kwani wameshindwa kutumia umaarufu wa Kikwete ili kuteka soko la kuuza sera za chama?
  The unseen is illustrated by the seen.
   
 13. F

  Froida JF-Expert Member

  #13
  Jun 13, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Umenifanya nitafuta kikombe cha maji ninnywe manake nimecheka mpaka sina mbavu Kweli JF ni kiboko cha njia ,yaani waalimu wanasaidia kuisindikiza CCm kaburini
   
 14. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #14
  Jun 13, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  CCM haijafa, ila imekaribia kufa. Na kama unavyojua anayekaribia kufa huwa ni msumbufu sana.
  We sikia, Mara Lowassa kasema kuna siasa za Makundi, Mara Rostam kasema Siasa uchwara, Mara Mwakyembe kababuliwa ngozi na kundi hili, Mara Masha kaja na lake eti vijana hawaipendi ccm kwa sababu hawajui historia, Mara Deo naye kaja na la kwake, Mara Membe naye kaja na lake, njia nyeupe kwa waungwanaa!
  Nitashangaa kama kuna mtu bado anaamini ccm ipo imara!
  Kasome kalamu ya mwigamba
   
 15. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #15
  Jun 13, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Itawachua muda mrefu sana kukubali kuwa CCM imekufa, hata mwaka 2015 hamtaamini maramoja kuona hamko madarakani! Hayo mengine ni kuwayawaya tu!! Au, hutaki?!... .....
   
Loading...