CCM imejipanga kushughulikia mamluki ndani ya chama

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
KATIKA uchaguzi mkuu uliopita, wagombea urais walitoa ahadi mbalimbali ili kuvutia wapiga kura.

Pamoja na mambo mengine, wagombea wawili walijinadi kwamba wakiingia Ikulu watatoa elimu bure. Wagombea wengi wa urais walijinadi pia kwamba watasimamia uchumi wa nchi kwani suala la elimu bure, kwa mfano, maana yake ni mzigo wa elimu kuchukuliwa na serikali na hivyo inahitaji kuwa na uwezo huo. Mgombea wa upinzani kupitia Chadema, Edward Lowassa aliahidi kutoa elimu hadi Chuo Kikuu, wakati yule wa CCM, Dk John Magufuli alisema serikali yake itatoa elimu bure hadi kidato cha nne.

Watanzania wengi walikuwa wanaona kama ahadi hizo zilikuwa za kuombea kura tu majukwaani, hususani suala zima la elimu bure, mintarafu ukubwa wa nchi yetu na ongezeko la watu. Na wengi waliamini, kama utoaji wa elimu bure utaanza basi ungelichukua muda huku kukiwa pia na visingizio hivi na vile, lakini hali imekuwa tofauti baada ya kupata serikali mpya. Serikali ya Awamu ya Tano iliyoanza kazi siku hiyo hiyo baada ya kuapishwa imethibitisha kwamba haina utani katika kutekeleza ahadi zake.

Ni kutokana na hilo, makundi mbalimbali nchini yameendelea kuipongeza Serikali ya Rais John Magufuli kwa kutimiza ahadi zake, tena katika kipindi kifupi tangu alipoingia madarakani Novemba 05, mwaka jana ikianza na inayogusa jamii kubwa, elimu bure. Lingine linalokwenda sambamba na hilo na kuwahakikishia Watanzania kwamba watoto wao kweli watasoma bure na siyo nguvu ya soda ni ukusanyaji wa kodi ambapo katika kipindi kifupi serikali imekuwa ikikusanya zaidi ya Sh trilioni 1.4 kwa mwezi.

Kinachoelezwa na wananchi ni kwamba sera ya elimu bure, ingawa bado ina changamoto nyingi, lakini ingetekelezwa kwa kusuasua sana kama Rais Magufuli asingekuwa jasiri katika kutumbua majipu na vijipele tangu alipoingia madarakani, Novemba 05 mwaka jana. Katika kutekeleza mpago wa elimu bure, Watanzania wameshuhudia serikali ikisambaza zaidi ya Sh bilioni 18 mashuleni.

Kinachojidhihirisha ni kwamba kabla Serikali haijaondoa ada na michango mingine lukuki, wazazi wengi walipata ugumu katika kuwawezesha watoto wao kwenda shule kutokana na uduni wa vipato na baadhi ya vijana ambao wako mtaani ni matokeo ya kukosa ada. Kwamba kama wangekuwa shule zama hizi za Magufuli baadhi yao wangefika chuo kikuu!

“Mimi kama mzazi kikwazo kikubwa kwangu kilikuwa kuwalipia ada watoto wangu wawili ambao walikuwa wakisoma katika shule za sekondari za umma. Nilipaswa kulipa ada ya Sh 20,000 kwa kila mmoja wao lakini hali ilikuwa zaidi kwenye michango. Wastani kwa mtoto mmoja ilifikia hadi Sh 180,000 kwa mwaka ambazo sikumudu,” anasema John Sikazwe, baba wa watoto sita, mkazi wa kitongoji cha Kizwite, Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa Anaongeza: “Kwa kweli nilishindwa kuwalipia ada na michango mingine wanangu ingawa walifaulu na hivyo watoto wangu wote wawili walishindwa kuendelea na masomo.

Mmoja alikuwa aingie kidato cha tatu na mwingine aliacha shule akiwa kidato cha kwanza, tena katika muhula wa kwanza.” Anasema watoto wake hao kwa sasa wanajishughulisha na kutoa huduma za usafiri katika Manispaa ya Sumbawanga ambapo mmoja ni dereva wa pikipiki ya magurudumu matatu (bajaji) na mwingine ni dereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda.

Anasema wakiwaona wenzao waliohitimu sekondari na vyuo vikuu wanasikitika sana kwa kuwa uwezo wa kusoma walikuwa nao isipokuwa uwezo wa kifedha uliwafanya watoke shuleni. Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Clifford Landari, anakiri kuwa ulipaji wa ada shuleni, ulifanya wazazi wengi kushindwa kuwalipia watoto wao, hali anayosema kuwa ilifikia wastani wa watoto milioni 3.5 kukosa elimu hiyo ya msingi.

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, elimu bure kuanzia mwaka huu itarudisha watoto hao waliokosa elimu darasani. “Naipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutimiza ahadi ya kutoa elimu bure, hata kama katika hatua hizi za mwanzo kutakuwa na upungufu wa hapa na pale, lakini mpango huu ukifanikiwa utaongeza wigo wa watoto kwenda shule,” anasema Mkuu wa Shule ya Sekondari Kalangasa, Manispaa ya Sumbawanga.

Wananchi, wakiwemo wazazi na walezi waliohojiwa na mwandishi wa makala haya kwa nyakati tofauti mkoani Rukwa wanawataka wakurugenzi, maofisa elimu wa mikoa na wilaya na wadau wengine wakiwemo wakuu wa shule za sekondari na msingi kuwa bega kwa bega na Serikali ya Awamu ya Tano katika kutekeleza mpango wa elimu bure kwa moyo mnyoofu na kuhakikisha unafanikiwa.

“Tunasema hivyo kwa sababu wapo baadhi ya wakurugenzi nchini ambao wamenukuliwa wakitoa nyaraka ambazo zinakinzana na agizo hilo la serikali ikiwemo michango mbalimbali,” anasema Aidan Mwakoma, mkazi wa kitongoji cha Chanji – Kisiwani, Manispaa ya Sumbawanga. Wananchi hao pia wanapongeza juhudi za mawaziri kwa kuonesha kwa vitendo pale ambapo kunajitokeza kasoro za kiutendaji, ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua watendaji wanaoonekana kukwamisha mpango huu wakiwemo wakurugenzi.

Ukusanyaji wa zaidi ya Sh trioni 1.4 kwa mwezi nao umeendelea kupongezwa na wananchi kwa ukusanyaji huo wa mapato mengi. Miongoni mwa waliojitokeza kumpongeza Rais Magufuli ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania, Johnson Minja. Anasema hayo ni matokeo chanya ya ushirikiano kati ya serikali na wafanyabiashara ambao wapo katika sekta binafsi katika kuhakikisha kwamba kodi ya serikali inalipwa kwa mujibu wa sheria na kisha inaingia kwenye mkondo rasmi wa serikali.

Anasema ushirikiano huo chanya kati ya serikali na wafanyabiashara hauna budi kudumishwa kwa manufaa ya pande zote mbili na wananchi kwa ujumla kwa sababu kadiri kodi inavyozidi kukusanywa na kuingizwa katika mikondo rasmi, nchi itaweza kupata ustawi na kujiletea maendeleo. “Tunamshukuru Dk Magufuli kwa kuonesha ushirikiano pamoja na sisi, kwani ameamini kuwa nchi inaweza kujiletea maendeleo kwa kushirikiana na wafanyabiashara ambao ni sekta binafsi na matokeo ya ushirikiano yamezaa matunda,” anasema Minja.

Anasema kipindi cha nyuma, fedha nyingi za kodi zilikuwa zikiingia kwenye mifuko ya watendaji wasiokuwa waaminifu badala ya kwenda serikalini kwa ajili ya umma. “Wafanyabiashara si kwamba hawataki kulipa kodi, tatizo ni kwamba kodi nyingi zilikuwa za usumbufu na pia watendaji wa mamlaka za ukusanyaji, walikuwa wakijipatia fedha kwa maslahi binafsi, lakini Dk Magufuli ameliona hilo na amewashughulikia wale waliokwepa kodi na kuwashirikisha wafanyabiashara,” anasema Minja.
 
Back
Top Bottom