Ccm imedumaa kifikra na kimtazamo

Ccm imedumaa kifikra na kimtazamo

Nikukumbushe

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2013
Posts
2,602
Reaction score
409
Katika matukio ya mauaji na utesaji unaoendelea hapa nchini,viongozi wa ccm na serikali wamekuwa wepesi kutaja kuwa chadema wanahusika kwa mfano:
-Tukio la kuteswa kwa Dr ulimboka,ccm na serikali yake walisema kuwa mgogoro wa madaktari unachochewa na chadema,kama ndiyo walikuwa wachochezi mbona hamkuwakamata?
-Tukio la kuawawa kwa Mwangosi walisema chadema,sasa najiuliza kama muuaji mnamjua si mmkamate? Kuna haja gani ya kufanya uchunguzi?
-Tukio la kutekwa kwa kibanda pia walisema chadema wanahusika,huku wakitamba majukwaani kuwa wanao mkanda unaonesha chadema wakipanga mauaji,je leo hii imefikia wapi? Ushahidi wa duniani na mbinguni uko wapi?
-Tukio la mlipuko wa bomu Arusha,tuhuma zinakwenda kwa Chadema,lakini nashindwa kuelewa kama chadema ndio wanahusika si wawakamate? Kuna haja gani ya kufanya uchunguzi wakati wauaji wanajulikana?
-Na mengine mengi yanayofanana na hayo.
Kiuhalisia,Ccm huwa wanawatuhumu bure chadema ili kuonekana wasafi,lakini matukio haya yote wanahusika.Nasema hivyo kwa sababu kila kauli inayotolewa na viongozi wa serikali na chama cha mapinduzi,lazima jambo kubwa litokee.Hii ni dhahiri kuwa mambo haya yanapangwa kabisa.Ni mwendelezo wa upuuzi ule ule kutoa dau kwa atakayefichua mlipua bomu wakati wao kwa akili zao ndogo wanajua mhusika wa bomu,sasa dau ni ya nini wakati muuaja anajulikana?
 
Back
Top Bottom