mie niko Igunga tunavyoongea hivi, acheni kupotosha watu kuwa hapa kuna udini, naomba kwanza uelewe kuwa wakazi wa wilaya ya Igunga asilimia 75 ya wakazi wake ni wasukuma ambao wengi wao hawana imani ya hizi dini za kigeni, kuna waarabu kidogo tu hapa Igunga mjini ambao hata hivyo diwani wake ni wa Chadema , CUF hawana hata diwani jimbo zima hili na mikutano yao wanafanyia uchochoroni kama ambavyo mwenyekiti wao amekuwa akifanya
Sasa mziki upo cuf watabaki kuwa kama mbatia tu pale kawe, CCM wanaweza kusumbua kidogo maana bado wanamtaji wa wenyeviti wa mikoa , ila kwa mwitikio huu wa CDM , sioni kitakachozuia tusichukue jimbo kama tu tutasimamisha mgombea makini