Ndugu zangu kwa mujibu wa katiba1977 iliotungwa na Ccm hawahawa ktk ibara ya13 inaeleza wazi hakuna alie juu ya sheria, inashangaza leo hii nchi inaendeshwa kwa matamko badala ya katiba. Hofu yangu ni kwamba kesho tutachukiana wenyewe na mwisho majuto atakua mjukuu naona chuki zinaongezeka kati ya upinzani na CCM,jamii kwa jamii tuendako naona giza nene, nawakumbusha CCM hii nchi ni ya watanzania wote na sio mali ya CCM. Tusisahau kinga ni bora kuliko tiba,tusijekumbuka shuka kumekucha.