CCM huwa wanamuogopa Rais?

Kama unaona muuliza swali ataandaliwa Basi nakushauri uende wewe uulize swali lolote siku mh Rais akipita eneo lako, halafu uone Kama utakosa majibu ya kutosha, maswali gani yaishinde Taasisi ya Urais kuyajibu, Hivi kwa fikra zako Kwamba Rais akose majibu yaulizwayo na wananchi, Embu yaweke hapa hayo maswali tuyaone maana hapa wanapita viongozi wetu
 
Nani hakuingia madarakani kihalali, si ungeweza kwenda mahakamani kufungua kesi, umekaa nyumbani hata kupiga kura hujaenda halafu unataka mgombea wako ashinde, Badala ya kupiga kelele ilitakiwa uhamasishe wenzio mwende mkapige kura,
Vitu vingine uwe unasoma tu na kutulia.Kama utaendelea kuwa unakaza shingo hata kwa ukweli unaousoma na uliushuhudia basi tegemea "mema" huko mbeleni.
 

Nikikwambia waulizaji wanaoandaliwa sibahatishi. Kiongozi gani anapita hapa? Weka jina lake tulione. Hakuna majizi ya kura yako tayari kuulizwa maswali.
 
Nikikwambia waulizaji wanaoandaliwa sibahatishi. Kiongozi gani anapita hapa? Weka jina lake tulione. Hakuna majizi ya kura yako tayari kuulizwa maswali.
Weka hayo maswali na siyo lazima ujuwe viongozi wapitao hapa maana unachohitaji wewe Ni majibu, Nami Kama mwananchi na kijana mzalendo ninayeifuatilia serikali yangu katika utendaji wake wa kazi naweza kukusaidia baadhi ya majibu

Maana unaweza ukakuta unaswali ambalo lilishatolewa ufafanuzi lakini wewe ukawa hukupata nafasi ya kusikiliza majibu ya dukuduku lako
 

Ww chawa huna uwezo wowote wa kujibu maswali ya msingi, kama viongozi wako hata wakisikia mdahalo wanakimbia itakuwa ww chawa? Ww endelea kuandaa vikundi vya kikatili vya kupora fomu wapinzani, na kuwateka wakati wa uchaguzi.
 
Utakuwa na mama wangapi wewe? Cheo kinakufanya uite mama yako wakati mama flan jirani yako hujawahi hata kumuita mama! Utakuwa mnyakyusa ww.
 
Ww chawa huna uwezo wowote wa kujibu maswali ya msingi, kama viongozi wako hata wakisikia mdahalo wanakimbia itakuwa ww chawa? Ww endelea kuandaa vikundi vya kikatili vya kupora fomu wapinzani, na kuwateka wakati wa uchaguzi.
Mdahalo gani uliweka huo, maswali gani hayo ambayo unashindwa kuyaweka hapa mtanzania mwenzangu

Pili chini ya mama Samia hakuna vikundi hivyo uvisemavyo wewe, Kama umeviona Nakuomba utoe taarifa kwenye vyombo vyetu vya ulinzi na usalama maana jukumu la ulinzi na usalama Ni jukumu la Raia wote wa Tanzania
 
Kwa nini siku hizi hamtangazi mapato ya tozo za miamala kama mlivyofanya hapo mwanzoni?
 
Utakuwa na mama wangapi wewe? Cheo kinakufanya uite mama yako wakati mama flan jirani yako hujawahi hata kumuita mama! Utakuwa mnyakyusa ww.
Anasifa zote za kuitwa mama,Na nikimwita mama Wala sijakosea kitu, Ni heshima,Ni upendo, Ni utamaduni wetu pia, lakini pia acha na ondoa kichwani mwako vimelea vya ukabila

Maana hivyo vitakupofusha uwezo wako wa kufikiria na kijikuta unajikuta Hilo, Zimwi la ukabila tulisha kushinda na usiturudishe huko ambako tulishatoka

Tubishane kwa hoja na siyo kabila, Na hata nikikosea Mimi siyo kabila linalokuwa limekosea
 
Mama flani jirani yako hana sifa zote za kumuita mama? Au ndo zile huongezewa?
 
Kwa nini siku hizi hamtangazi mapato ya tozo za miamala kama mlivyofanya hapo mwanzoni?
Miradi mbalimbali inayotokana na tozo inaendelea kuelezwa na kiasi chake Cha pesa, lakini pia utaratibu haujaachwa Bali utapata tu taarifa, hii Ni serikali ya uwazi inayoendeshwa kwa misingi ya Sheria na utawala Bora chini ya mh Mama Samia Suluhu Hassan, hivyo ondoa hofu endelea kumuunga mkono Rais wetu
 
Mnatuchota tu za nauli kwny helicopter na matembezi ya kugawa mitungi. Miradi si tunaona mikopo ndo inafanya kazi hyo
 
Mi ni jirani yako sema natumia unknown ID ndo maana hunitambui.
Inapendeza tumia jina halisi Kama Mimi maana ukitumia ID ndio maana mnatukana Sana kwa kuwa unajuwa huwezi ikajulikana, lakini ukitumia jina halisi inakuwa unajenga hoja kwa heshima busara na upendo bila kumvunjia mtu heshima, ndio maana kwa I'd unaamua hata kudanganya tu Kama ulivyo danganya
 
Ila yote kwa yote, uchawa ni mbaya sana! Kuijenga nchi kwa kutetea hata lililo baya ni dhambi hadi kwa vizazi vijavyo. Jitahidini mfungue mawazo chanya kwenye kupongeza mpongeze na kwny kukosoa mkosoe. Siyo baya mlitengeneze lionekane la mvuto. Hata rais ni mwanadamu hukosea msimchukulie km malaika wa heri.
 
Sisi penye kushauri tunashauri ili kuboresha na penye kusahihisha tunasahihisha Kama alivyo wahi andika kitabu chake Hayati baba wa Taifa mwalimu nyerere juu ya kujisahihisha, Rais wetu Ni mwanadamu na ndio maana tunataka mumkosoe kwa staha na heshima na siyo matusi

Rais wetu Ni msikivu na muungwana Sana, Ni muelewa na anashaurika vyema, Tuzingatie maadili yetu ya kitanzania katika kuheshimiana na kuheshimu utu wa kila mtu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…