CCM: Heko Rais Samia kupunguza tozo za miamala

Alipoweka tozo mlimpongeza na kumpa heko, amepunguza tozo mmempongeza na kumpa heko pia akifuta tozo mtampongeza na kumpa heko. Ninyi ni Makasuku?!🤡🤡🤡
 
Nini hapo cha kumsifia sasa , tatizo limetengenezwa na serikali yake na kubarikiwa na bunge la chama chake
 
Unajitekenya na kucheka mwenyewe halafu unampongeza kwa nguvu kubwaaa mchekeshaji! Dah
 
Huu ndio usheitwani tunaoukemea makanisani na misikitini.

Hata angeiondoa tozo yote hakupaswa kusifiwa kwani tozo haijaketwa na wazungu au Ibilisi.

Yaani hili ni sawa na mtu akugonge na gari akukimbie baadaye akuambie atachangia 30% ya gharama za matibabu nawe unashangilia.
Fyuuuu
 
CCM Ni mazwazwa kinoma asee... Mambo wanayofanya mpaka yanatia kinyaa...

Hivi kweli wanaamini bado tunaishi tz ya wajinga kiasi hicho?!... Au wao ndo wajinga kiasi hiki?!...

Wakope bhac akili kidogo toka kwangu badala ya hizi drama za kitoto wanazofanya... Hovyo kabisa yaani.

Kweli asee... Mbuzi anapokaribia kufa anapochinjwa huwa anarusharusha miguu...
 
CCM: Heko Rais Samia kupunguza tozo za miamala.

Na mwandishi wetu,
Dar es Salaam.

"Chama Cha Mapinduzi kinasifu na kupongeza msimamo imara na thabiti wa @ Rais Samia wa kujali na kuwasikiliza wananchi kushughulikia malalamiko yaliyotokana na makato makubwa kwenye miamala ya simu" Shaka Mwenezi Taifa.

"Punguzo la tozo hizo litaleta unafuu kwa wananchi ambao wengi wamekuwa wakitumia miamala ya simu kuendesha shughuli za kiuchumi na kusaidia wahitaji" Shaka Mwenezi Taifa.

"Uamuzi wa serikali umetolewa wakati muafaka ingawaje wananchi bado wana wajibu wa moja kwa moja kuchangia maendeleo ya Taifa" Shaka Mwenezi Taifa.

"Kitendo kilichofanywa na serikali ya Rais Samia ni cha kizalendo kwa kuwajali wananchi wake na kwamba ameonesha uungwana wa kiwango cha juu kusikiliza kilio cha wananchi na kutekeleza matakwa yao" Shaka MweneziTaifa.

"CCM inampongeza @ Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwasikiliza wananchi kuhusu sakata la tozo za miamala ya simu ambapo alitoa maelekezo ya viwango hivyo kutazamwa upya na sasa imepunguzwa kwa asilimia 30 huku makampuni yakipunguza kwa asilimia 10" Shaka Mwenezi Taifa.

"Kazi ya kujenga nchi ni wajibu wa watanzania wote bila kujali itikadi za kisiasa. Uamuzi huu ni upendo mkubwa alionao kwa wananchi anaowaongoza ili washiriki kuchangia maendeleo ya nchi yao kwa furaha" Shaka Mwenezi Taifa.

"Hata hivyo kila mwananchi anatakiwa kuelewa kazi ya ujenzi wa nchi, kuweka msukuko wa maendeleo na shime ya upelekaji huduma za jamii katika maeneo yote ni kazi na jukumu la kila mwananchi kwani serikali ni watu na watu ndiyo wananchi wenyewe" Shaka Mwenezi Taifa.

"Watendaji wote dhamana ni vyema kuelewa kuwa kazi ya kumsadia Rais katika kila eneo ni wajibu usiohitaji kuelekezwa wala kusukumwa badala yake kila mmoja atimize wajibu wake ipasavyo wakiweka mbele maslahi ya umma" Shaka Mwenezi Taifa.

" Niwasihi watanzania kupuuza uvumi unaoenezwa mitaani kuwa serikali ina mpango wa kusitisha elimu bila ada kwenye jambo hilo serikali ya Rais Samia imejipanga vizuri sana kuhakikisha elimu inatolewa bure na yenye viwango" Shaka Mwenezi Taifa.

"Serikali ya Rais Samia itaendelea kugharamia mpango wa elimu bila ada kwani unawagusa na kuwanufaisha wananchi walio wengi hivyo hila zozote za kutaka kuichafua serikali hazitafanikiwa " Shaka MweneziTaifa.

"Serikali ya Rais Samia zaidi itaendelea kutatua changamoto zilizokuwa zikikabili mpango huu ili wanafunzi wakitanzania wapate elimu katika mazingira mazuri zaidi. Hivyo niwaombe wananchi wapuuze taarifa zinazodai serikali itausitisha." Shaka Mwenezi Taifa.

"Usikivu, Unyenyekevu, Busara, Ustahamilivu na Utayari wa Rais Samia Suluhu Hassan imekuwa suluhisho sahihi kwenye uongozi wake hasa katika utatuzi wa kero za wananchi kweli ni (MAMA SULUHU)" Shaka Mwenezi Taifa.
😍👋💪
 
Back
Top Bottom