CCM hawabebeki: STAR TV (Diallo) wawatosa kurusha uzinduzi wa kampeni Arumeru live

chachana

Member
Aug 4, 2011
57
92
CCM walipanga kurusha uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa arumeru live kupitia STAR TV, imethibitila imeshindikana. Kushindikana huku pamoja na kuwa mmiliki wa kituo hicho ni kada wa ccm kunatokana na sababu nyingi za kibiashara lakini kubwa ni kuwa ccm haibebeki.
Inasemekana mara nyingi ccm wamekuwa wakitumia shuruti za chama tawala kwa kutaka mara kadhaa matukio yao yarushwe bure. Pamoja na hilo, makada wengi, wafanyabiashara na hata wananchi wa kawaida wengi wamechoka kujitolea kukisaidia chama hicho kwa vile hakina mvuto tena, kitu ambacho kinatoa tafsiri ya anguko la ccm muda si mrefu.
 
Wanapenda kurushiwa bure huku wanatoa posho kibao kwa wahudhuriaji!
ama kweli kuitetea sisiem inahitaji kuwa na akili ya maiti
 
Hivi MAMILION wanayopata CCM kila mwezi kwa kuwa na wabunge wengi, wanayatuiaje? Tukio kama hili si ingekuwa ni njia mwafaka wa kutumia hizi fedha? Si ni kutaka kumantain namba yao ya wabunge.
Wana janmvi, napenda kujua: Hivi Chama kikipoteza namba/idadi ya Wabunge waliokipa idadi fulani ya Viti Maalum, kinaPUNGUZIWA (kisheria) Wabunge wake wa Kike?
 
ukiwaendeza gambaz kama una mradi wako lazima ufe..kwenye skendo ya ku collapse shirika la ndege ATC, ccm wamehusika sana utasikia tuwekee siti nne kuna wajumbe wanaenda mwanza kwenye mkutano..tutalipia..hapo ndio ujue imetoka..
 
1-4-2012 cku ya wajinga, wa Arumeru kwa kutokuwa wajinga chagueni ccm na kama mtakuwa wajinga chagueni upinzani,, hao wapinzani bd ni kimvuli hawana nguvu ya kutekeleza hata jambo moja ktk maendeleo yenu ila kama mnataka cku ya kujifurahisha kwa cku moja chagueni upinzani mkitaka mtimize malengo ya maendeleo ya jimbo lenu chagueni ccm.
 
Kurushiwa matangazo unalipwa au unalipa?
Star Tv ndio wangewalipa CCM na sio kinyume.
 
ukiwaendeza gambaz kama una mradi wako lazima ufe..kwenye skendo ya ku collapse shirika la ndege ATC, ccm wamehusika sana utasikia tuwekee siti nne kuna wajumbe wanaenda mwanza kwenye mkutano..tutalipia..hapo ndio ujue imetoka..

kama ulikuwepo aiseee
 
Back
Top Bottom