CCM hali mbaya kiuchumi? Uhai wake u mwishoni

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Sitaki kuamini kwa chama kikubwa tena chenye dola kulialia mapaka kufikia kuahirisha kikao kwa sababu ya ukata wa fedha! Inawezekanaje kwa chama kikubwa tena chenye rasirimali kibao kilichijilimbikizia wakati wa chama kimoja kulia hakuna pesa? hii ni aibu!


Hii sio dalili nzuri kwa upande wa ccm, inawezeka kabisa kua chama hiki ndio muda wake wa kukata roho, inaonekana chama kimekosa wasimamizi wazuri wa rasilimalizi hizo kila moja amawazia tu tumbo lake, hii ni zaidi ya aibu iliyopitiliza. Nilitegemea vyama vichanga kulilia lia lakini sio chama cha maapinduzi.


Hiki ni kiashiria kua chama hiki kikongwe ambacho ni umri wa mzee kwa sasa kufikia ukingoni, ni kweli kabisa mtu ukishafikia uzeeni ndio unakaribia kaburini! Kwahiyo ccm pumzi kwisha, uzee wa chama ni tatizo, chama nimechoka kimebaki kujifia hakuna namna!


Ukiangalia ya Zanzibar na chaguzi mbali mbali za mameya zilizofanyika huko siku za nyuma utaona kua chama kimekosa hoja kimebaki kutumia ujanja ujanja na ubabe kusalia madarakani! huku ni kukosa pumzi. Chama badala kujikubali kua kimeshindwa ili kujisahihisha na kujipanga upya ili kurejea madarani badala yake ni ujanja ujanja usiokua na maana. CCM upande wa Zanzibar imekwishafutwa hili halina ubishi kabisa, kutokuwepo kwa CUF katika utawala huu hakumaanishi kua ccm ndio imepata nguvu mpya bali ndio kifo kimewadia, nina imani kwa sasa uitishwe uchaguzi huru na wa haki Zanzibar kwa sasa CCM hawawezi kupata kiti hata kimoja! anayebisha Mungu ampe uhai afike siku zijazo.
 
Hizi ni Akili za Mgonjwa aliyelazwa ICU anapoombea Daktari bingwa aliempeleka ICU afe ili yeye aweze kutolewa huko
 
Kiongozi, salaaam!

Haya yatabaki kuwa mawazo yako CCM iwe zanzibar au bara iko madhubuti sana na hakuna chama cha siasa kitakachokaribia hata kwa 38% - "Wacheni waandamaneee, CCM mbele kwa mbele"
 
Kiongozi, salaaam!

Haya yatabaki kuwa mawazo yako CCM iwe zanzibar au bara iko madhubuti sana na hakuna chama cha siasa kitakachokaribia hata kwa 38% - "Wacheni waandamaneee, CCM mbele kwa mbele"
CCM upande wa Zanzibar imekwishazikwa! Waliopo ni mawakala wa bara!
 
hahahahaha ccm ccm ccm ccm hahahaha mapoyoyo ya lumumba yanaisoma number .juzi Mwenyekiti wao kageuka kuwa muse7n hataki kuachia uwenyekiti hahahaha yapo pale lumumba hayana kazi na bado.

swissme
 
Wauze viwanja vya mpira vya Majimaji Songea,Samora Iringa,Sokoine Mbeya na Ally Hassan Mwinyi Tabora ili wapate billioni 2 za kufanyia mikutano mkuu maalum.
 
Wauze viwanja vya mpira vya Majimaji Songea,Samora Iringa,Sokoine Mbeya na Ally Hassan Mwinyi Tabora ili wapate billioni 2 za kufanyia mikutano mkuu maalum.
Kama ela itakuwa haitoshi wauze pia ofisi ndogo ya makao makuu Lumumba.
 
Asijua maana haambiwa maana. Kaa ukisubiri mkono wa fisi uanguke.

Mlizoea kuLugumi eh???Safari hii lazima muisome tu.............Chama Cha Majipu.............Naona hata kukaa hamuwezi jinsi kila mahali panamshona wa kutumbuliwa.............Mpaka Mwenyekigoda ameamua kustisha kutoa kigoda.................
 
Asijua maana haambiwa maana. Kaa ukisubiri mkono wa fisi uanguke.
Wale wafanyakazi wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo hamjawalipa tangu Novemba mwaka 2015, mnadhani wanaishi vipi? Walipeni banaaa. Acheni porojo
 
CCM inashikiliwa na Pombe tu otherwise ilishakufa na akipewa uenyekiti anaiuwa na asipopewa ndiyo anaiangamiza jumla
 
kwani wale mafisadi waliokuwa mstari wa mbele kuchangia ccm wako wapi? wametumbuliwa au wanaogopa kutumbuliwa?mzoea vya kunyonga vya kuchinja haviwezi. na bado subirini mtumbua majipu akiwa mwenyekiti wa chama.wachumia tumbo watahama wote hapo lumumba.na hapo ndipo tutaheshimiana humu Jf.
 
Kiongozi, salaaam!

Haya yatabaki kuwa mawazo yako CCM iwe zanzibar au bara iko madhubuti sana na hakuna chama cha siasa kitakachokaribia hata kwa 38% - "Wacheni waandamaneee, CCM mbele kwa mbele"
Nyie ndiyo mliotufanya mpaka sukari tunanunua kg1 sh.3000
 
Masifia ccm chama lenu halina mahera ya mkutano mkuu, haya sasa michango kama ya mwenge mkichangie chama mmekifilisi wenyewe. Mamiziki, masinema, mavichekesho haya sasa si mlifurahi, matajiri mliwaita wezi wamekula kona na mkicheza hata yale matisheti itakuwa kumbukumbu kama vile magwanda ya chipukizi enzi hizo. Yale matisheti chagua magufuli msiyatupe chaguzi zijazo ziwafae ccm kwishney ya sheby kisu kondoaaaa
 
Ningeshangaa kama miradi ya chama ingekuwa inaendelea vizuri wakati mafisadi papa serikalini ni vigogo wa CCM
 
Back
Top Bottom