Serekali 3 ni kifo kwa ccn.
ccm ilikuwepo ipo na itaendelea kuwepo
CCM ilishanoga kama mlenda siku nyingi wanasubiri walaji tu!!
umeandika ukweli mtupu ! Ccm imejinasisha yenyewe ! Lakini tuliwajulisha mapema sana kuhusu hili .
hatuongelei wafu wa c.c.m,tunaongelea juu ya katiba mpya na serikali tatu!
Tatizo letu ni kujifanya kutokuona chanzo cha KUJIKWAA na kubaki kulaumu pale TUANGUKIAPO.Hali ni mbaya upande wa ccm baada ya hila zake za kuchakachua rasimu ya katiba iliyowasiliswa na Tume ya Jaji Joseph Warioba kubainika.
Imebainika kwamba kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba, 2012, waliojitoa kwenye bunge maalumu la katiba ni ccm.
Kujitoa kwa ccm kisheria kunatokana na uamuzi wao wa kuachana na rasimu iliyowasilishwa na Tume na kuamua kujadili rasimu iliyowasilishwa na kikundi fulani cha ccm kinyume cha sheria ya mabadiliko ya katiba.
Aidha kauli za baadhi ya makada wa ccm ambao wameonyesha kukerwa na hila hizi na kuweka wazi kuwa itakuwa ngumu katiba kupatikana bila UKAWA, kauli ya msajili kuwataka ccm warejee kwenye rasimu ya warioba, na ukimya wa walioandaa rasimu ya ccm vinaashiria hali ni mbaya ndani ya ccm.
Hivi sasa kuna mnyukano ndani ya ccm ambapo wakongwe wanadai hakukuwa na haja ya kuigharimu nchi kwa kuanzisha mchakato wa katiba na mwisho wa siku kuyakataa maoni ya wananchi.
NB
Tujadili bila kuweka ushabiki wala itikadi.
Hili ni suala la kitaifa.
Tatizo letu ni kujifanya kutokuona chanzo cha KUJIKWAA na kubaki kulaumu pale TUANGUKIAPO.
Mkuu, TEC inajua fika kuwa UKAWA ni WANANCHI ila sijui kuna nini kinachofanya kila mtu awaseme UKAWA kana kwamba ndio CHANZO cha BMK kukwama. Wengi hawasemi na kuilaumu CCM kwa kusababisha hali hii kwanza kwa kutoijadili Rasimu ya katiba iliyowasilishwa na tume na pili lugha chafu waliyokuwa wakiitumia wabunge/jumbe wake mpaka kupelekea UKAWA kususia vikao. Kwanza aliyeanzisha UKAWA ni hao hao CCM.Kuna hatari ya taifa kugawanyika vipande vikuu viwili.Tayari taasisi za kidini hasa Roman catholic wamebaini makosa yao ya awali. wiki jana tumeshuhudia U-TURN kali kutoka TEC baada ya kutoka sauti ya individual bishops wakilaumu ukawa bila kujua kuwa ukawa ni wananchi.
Kuna vitu viwili ambavyo ni sahihi na ccm wanaviogopa sana ; Serikali moja na serikali tatu
1. Serikali moja - ilikuwa muafaka sana. Ila wanaiogopa Zanzibar.
2. Serikali tatu - wanaogopa kuondoa dhana ya chama kushika hatamu.
Hali hiyo imewafanya wapiganie serikali mbili ambazo sio sahihi kwa kuwa Tanganyika inapoteza utaifa wake