CCM haina dira, sasa yalamba matapishi yake ya 2010

CCM haina dira, sasa yalamba matapishi yake ya 2010

MSHINO

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2013
Posts
1,069
Reaction score
713
TANGU kuanza kwa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa 2010, kumekuwa na mjadala mahsusi kuhusu sera ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ya kutoa elimu bure kuanzia ngazi ya chekechea hadi kidato cha sita.

Sera hii imepingwa na kuzomewa vikali na Chama cha Mapinduzi (CCM). Binafsi awali sikutilia manani upinzani wa kutoa elimu bure kwa sababu ulitolewa na Kampeni Meneja wa chama hicho, Abdulrahmani Kinana, nikidhani kwamba alifanya hivyo kwa sababu za kisiasa na kipropaganda ukizingatia kwamba vyama vya siasa viko katika ushindani mkubwa wa kuomba ridhaa ya wapiga kura.

Hata hivyo, nimeanza kutilia manani upinzani huu baada ya Rais Jakaya Kikwete naye kujitokeza hadharani kupinga sera hii na kuungwa mkono na aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta. Upinzani wa sera hii kutoka kwa viongozi hawa wakuu katika nchi yetu umetia uzito wa kipekee hoja ya kwamba elimu bure haiwezekani kutolewa katika nchi maskini kama Tanzania.

Bila kufafanua dhana ya kutoa elimu bure na uwezekano wake, wananchi wataanza kuamini kwamba hili ni jambo lisilowezekana hasa watapoambiwa na viongozi wa chama tawaka na serikali yake. Ufafanuzi huu ni muhimu ukizingatia kuwa tupo katika jamii ambayo imejengwa katika mfumo wa kipropaganda wa kuamini au kuaminishwa kuwa chochote kinachosemwa na viongozi wa serikali na chama tawala kuwa ni kweli.

Aidha bado kuna watu katika jamii yetu ambao hutilia shaka chochote kinachosemwa na viongozi wa vyama vya upinzani na wanaharakati wengine, bila kuzingatia mantiki ya hoja.

Pengine kabla ya kufafanua juu ya uwezekano wa kutoa elimu bure, ni vizuri kuweka kumbukumbu sawa. CCM wana historia ya kupinga sera zenye kujaribu kuwapunguzia wananchi makali ya maisha, na hawajaanza na hili la elimu bure.

Itakumbukwa kuwa mwaka 1995 wapinzani waliahidi kufuta kodi ya kichwa (CCM waliita kodi ya maendeleo) ambayo ilikuwa inaleta adha kubwa kwa wananchi hadi wengine kufikia hatua ya kujificha porini ili wasikamatwe na askari mgambo.

CCM walipinga vikali sera hii wakisema kuwa haiwezekani kuendesha serikali bila kodi hiyo. Hata hivyo, baada ya uchaguzi mkuu wa 1995 serikali ya CCM iliifuta kodi hii, aghalabu kwa shinikizo.

Mwaka 2000 wapinzani walikuja na sera ya kufuta ada katika shule za msingi kama njia ya kuwawezesha watoto wengi zaidi kujiunga na elimu ya msingi. Kama kawaida yao, CCM walicharuka tena wakidai kuwa wapinzani wanaota ndoto.

Hata hivyo baada ya uchaguzi wa 2000 ada katika shule za msingi ilifutwa, japokuwa kwa shinikizo kubwa la Benki ya Dunia. Kwa hiyo, kwamba CCM leo hii wanapinga vikali tena bila aibu sera ya elimu bure sio jambo la kustaajabu.

Pengine jambo pekee la kustajaabu ni kwamba wapinzani wa sera ya elimu bure ni viongozi wa chama kinachojiita cha kijamaa. Haingii akilini hata kidogo kwa kiongozi wa chama kinachojiita cha ujamaa kupinga sera ya kutoa elimu bure. Msingi wa ujamaa ni usawa na fursa kwa wote.

Wana ujamaa popote walipo wanakubaliana kwamba njia rahisi ya kufikia usawa na kutoa fursa kwa kila mtu ni kuhakikisha kwamba elimu na huduma zingine za jamii zinamfikia kila mtu. Ili kutimiza hili, wana ujamaa wanakubaliana pia kwamba ni muhimu na lazima kwa huduma hizi kugharamiwa na serikali bila wananchi kuzilipia moja kwa moja.

Hii ni mantiki ya msingi ya ujamaa ambayo mwanachama wa kawaida wa chama kinachojiita cha kijamaa anapaswa kuielewa, achilia mbali kiongozi wake.

Wapinzani wa sera ya kutoa elimu bure wametumia kigezo cha gharama katika kuhalalisha upinzani wao. Kwamba haiwezekani kutoa elimu bure kwa sababu kufanya hivyo itamaanisha serikali iache kutekeleza majukumu mengine ya msingi.

Katika makala hii ninaonyesha kwa ufupi sana jinsi ambavyo inawezekana kwa serikali kulipia gharama ya elimu kwa kutumia fedha za walipa kodi bila kumbebesha mzazi gharama za ziada.

Katika kufanya hivi nitaenda hatua kwa hatua, nikianzia na kufafanua dhana ya elimu bure kwa mazingira ya Tanzania, na kubainisha vyanzo mbadala vya mapato kwa serikali ili iweze kulipia kikamilifu gharama za elimu na huduma zingine za jamii.

Chanzo:Tanzania Daima

 
Kudos Mshino; CCM is a dead party full of dead woods and recycled leadreship; utashangaa kuona yale waliyoyaweka kwenye ilani yao ya uchaguzi kama mahakama ya kadhi hawayatekelezi kabisa na kamati zao kule Dodoma zimepigilia msumari wa mwisho kwamba hakuna kuingiza mahakama ya kadhi kwenye katiba; sasa wamerukia ya wenzao kama katiba mpya (Sera ya Upinzani); yamewashinda sasa wamehamia kwenye elimu ya bure (Sera ya upinzani) ambayo waliiponda kwa bidii zao zote; sasa tusemeje hicho chama kipo kweli na kina viongozi weledi au dead woods?!
 
  1. Ilani ya CCM haikuwa na hoja ya katiba mpya na walitumia nguvu kubwa kupinga kuandikwa kwa katiba mpya lakini leo wanajifanya kuipigia upatu na kuishabikia! Katika Ilani ya CHADEMA, katiba mpya ilikuwa kilio chao!
  2. Dr. Slaa aliwaahidi wananchi katika kampeni zake kuwa angetoa elimu bure, lakini CCM walipinga na kudai haiwezekani! Leo hii Mwenyekiti wa CCM, Bw. JK ameona inawezekana na sasa yuko mbioni kuanza kutekeleza kutoa elimu bure!
  3. Dr. Slaa aliwaahidi wananchi kuwa angepunguza bei ya pembejeo na vifaa vya ujenzi kwa kupunguza kodi! Nadhani CCM wana-trot kutekeleza hija hii!
Nashauri CCM waweke kapuni sera na ilani yao ya uchaguzi wa 2010 waendelee kutekeleza ilani ya CHADEMA!
 
Taasisi yoyote yenye dira aka vision haikurupuki kufanya maamzi, na hili ni tatizo katika nchi yetu kwani yaliyo kwenye mipango huwekwa kando, kiongozi akiwa kwenye ziara akapokewa vizuri akapewa pilau na nyama choma basi anapandwa na mzuka anafanya maamzi makubwa peke yake so longer yeye ni mkubwa. Huwezi kuongoza taaisis kubwa km ikulu kwa kuamka asb ni kuamua lolote. CCM imeaacha kutekeleza yaliyo kwenye strategic plan zao km mahakama ya kadhi, kilimo kwanza, maisha bora kwa kila mtanzania sasa inatekeleza sera za vyama vya upinzania. Hasa hili la elimu bure walisema haiwezekani sasa wanasema inawezekana. nchi haiwezi kufika popote ikiwa chini ya mikono isiyo salama.
 
Kuna mtu aliyaona haya takribani miaka 10 iliyopita na kuwaambia waziwazi - je unakumbuka kilichotokea - shauri yako sisi hatumo!!!

Kukikosoa chama tawala lazima uwe na roho ya chuma!!
 
Mpaka mwaka 1993 elimu ilikuwa bure. Unapewa kalamu, daftati kasoro share za shule. Je, nchi ilikuwa tajiri?
Kwa sasa tunaambiwa na Rais wetu Kikwete kuwa uchumi umekuwa ukilinganisha na miaka yote baada ya Uhuru. Je, kwa nini ndo serikali ishindwe kuwalipia shule wanafunzi?

Anjo
 
Kweli kabisa Chadema waliipigia kelele katiba Maccm yameikumbatia bila AIBU Chadema walisema Elimu bure Maccm na Mkuu wao wameidandia hoja bila haya
 
Mbona kama makala hii imechelewa, Katibu mkuu wa CCM na Mwenyekiti wameshatangaza elimu bure hadi sekondari!
 
Back
Top Bottom