Ccm bingwa wa mbinu chafu!

Ccm bingwa wa mbinu chafu!

MTA1

Member
Joined
Jun 1, 2013
Posts
89
Reaction score
11
Asubuhi nilikuwa kijiweni Majimatitu Mbagala, ambako kulifanyika uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Mianzini, mgombea wa CCM akaibuka mshindi ambao ulitokana na mbinu chafu zinazoashiria CCM haiko tayari kuachia utawala nchini kupitia sanduku la kura.

Nimeona ni vizuri tukipeana taarifa namna CCM inavyotumia vibaya mamlaka za kiserikali kwa faida yao pasipo kujali maslahi ya watanzania wengine. Ikumbukwe kuwa kabla na wakati wa kampeni za udiwani, CHADEMA ilikuwa na ofisi katika eneo lililoko Kakonko Bar, ambako pia mikakati ya kampeni za CHADEMA zilikuwa zinaanzia pale.

Tofauti na CCM na CUF, vijana wengi na wasomi walioko katika kata ya Mianzini wanaipenda na wafuasi wa CHADEMA, pia Kakonko Bar ilikuwa ni kijiwe cha kukutania na kupangia mikakati ya ushindi. CCM baada ya kugundua CHADEMA ndiye mpinzani mkubwa kuliko CUF wakaamua kutumia mamlaka za serikali kupunguza nguvu za CHADEMA katani. Hatua ya kwanza ilikuwa ni kutumia maafisa wa Afya wilayani Temeke na Katani kutoa amri ya kufungia huduma za Kakonko Bar kutokana na kile kilichodaiwa kuwepo kwa mazingira machafu yanayohatarisha afya za wateja.

Baadaye inasemekana baadhi ya makada wa CCM walimfuata mmiliki wa Kakonko bar na kumpa siri kuwa kilichompoza ni kuwepo kwa ofisi ya CHADEMA ndani ya compound yake. Kilichofuatia ni mmiliki kutoa notisi ya kipindi kifupi CHADEMA wafungishe virago na pia kutoruhusu mikutano ya mikakati ya CHADEMA. Baada ya CHADEMA kuondoka siku ya tatu ofisi ya CCM ikafunguliwa ndani ya Kakonko compound tena ikafunguliwa rasmi na Mwenyekiti wa CCMM MKoa wa DSM, Madabida (Muuzaji ARV feki). Pia Kakonko Bar ikaanza huduma tena pasipo tishio la kufungiwa kutokana na mazingira machafu. HIYO NI CCM na matumizi mabaya ya madaraka

JE TUTAFIKA!!!!
 
Hawajaanza leo kufanya hayo

"To know the enemy is half the victory"
 
Kwahiyo chadema walikuwa wanategemea baa ili washinde uchaguzi?

Mshindwa hakosi visingizio...
 
Kwahiyo chadema walikuwa wanategemea baa ili washinde uchaguzi?

Mshindwa hakosi visingizio...

Ni aibu kwa chama ambacho kimepewa dhamana na wananchi kuongoza nchi na kusimamia rasilimali zote tulizopewa na Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, kwa zaidi ya miaka 50 sasa, kuendelea na mbinu chafu za kulazimisha ushindi wa wizi, vitisho hata pia kuua. Kwa sababu moja tu kubwa ambayo ndiyo leo inakitesa CCM, kushindwa kuendelea kuwekeza kwenye imani na roho za watu wake kwa njia ya kuwaletea maendeleo, ili waendelee kukipenda na kukithamini.
Wananchi wamekataa, na CCM kwa kutumia vyombo vya dola ambavyo wamewalisha baadhi ya wananchi kuamini kuwa ni mali yao ya kuendelea kuwalinda kuwa madarakani hata kwa maovu. Wanavitumia vyombo hivi kunyamazisha wananchi wenye mtizamo na mlengo tofauti badala ya kupambana na maovu ktk nchi.
Jeshi la Misri lilimwambia Morsi. Hatuwezi kuua raia wasiokuwa na hatia, na tuko tayari kufa kuwalinda. "We are ready to die to protect the people". Na hawakuwa tayari aidha kudhuru au kuua raia kwa kulinda uovu wa utawala.
Kuna siku Polisi na Wanajeshi watakataa kutumika kwa masilahi ya watawala, kwa sababu wanatokana na jamii ile ile ya uraiani ambako wazazi wao, watoto wao, familia zao na jamaa zao ndiko waliko. Na uwekezaji wao uko huko hauko angani.
Unataka kudumu ktk siasa , wekeza ktk imani na roho za watu wako. Ubabe, nguvu na hira havijawahi kuwa misingi ya kudumu ktk siasa. Bali ni chanzo cha machafuko ktk nchi. Ushauri wa bure.
 
Hizi ni porojo tu ambazo hazijibu swali la msingi kama chadema walitegemea baa ili washinde Mianzini.
 
Back
Top Bottom