CCM beki hazikabi

CCM beki hazikabi

Naitazama CCM ya JK kama timu ya mpira ambapo Golini yupo mzee mzima JK ambapo pamoja na umahiri wake wa kupiga dana dana mijadala ya kisiasa ni dhahiri kwamba atafungwa tu kutokana na beki wake no mbili bwana Billal kuwa bize sana na kuhudhuria misiba na kuwa mgeni rasmi kwenye funguzi za saccos...

Namba tatu akiwa bwana mkubwa Pinda ambaye hatujui kwanini kakabidhiwa no hiyo huku akiangushwa na no tano (kwa maana ya baraza zima la mawaziri) ambao jukumu lao lilitakiwa kufuta makosa ya watendaji wakuu wa serikali...

No nne tulitegemea sana wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha wanapambana na mipira iliyomshinda golikeeper na kumiliki mikiki mikiki ya mashambulizi ya upinzani ( Wananchi) kwa kuhakikisha wanasimamia haki...

No sita na nane ni watendani wa kada mabli mbali za serikali mfano ualimu,masuala ya kilimo na ufugaji ambao kama wangetabua majukumu yao hasa uwanjani wangehakikisha wanachezesha samba ambalo mashabiki wangekua na uhakika wa ushindi kwa maana ya maisha bora!

No saba haingekuwa na umuhimu sana ikiwa beki no mbili angesimama vizuri kwa kuwa nilitaraji angekuwa na uwezo wa kupanda na kushuka...

No tisa walistahili kusimama makada waandamizi wa chama ambao kazi yao kubwa ni kukaa na mabeki wa upinzani ili kuwamaliza kisaikologia na kuirahisishia no kumi na moja ya chama ambayo ni utekelezaji mzuri wa sera na ahadi kupiga mashuti golini huku watendaji wa serikali za wilaya na mitaa wakisimama no kumi kumalizia mipira iliyotemwa na golikipa wa upinzani wakati akipangua mashuti ya no 11..
..mkuu umetisha...suluhu ya ccm kusulubika ndo hii
 
CCM wanajua kushinda uchaguzi kwa mbinu yoyote ile. Wao sio kama CHADEMA wanaofurahia mikusanyiko ya wasikilizaji wa hotuba zao. Ninaifananisha CCM na timu ya football inayoshinda mechi kwa kufunga magoli kwa mchezo usiovutia wakati CHADEMA ni sawa na timu inayocheza mchezo mzuri uwanjani lakini inaishia kufungwa al maaruf CHENGA TWAWALA.
 
..mkuu umetisha...suluhu ya ccm kusulubika ndo hii

Ni mara nyingi sana kiranja wangu nimekuwa nasikia hutu tuneno tunakokasirisha....
Zamani kipindi hicho kalamu nyekundu na stapler ikitakiwa iwe ofisi ya mwalimu mkuu tu nilikuwa nikisikia neno upinzani nadhani ni sawa na uhaini na kwamba mpinzani ni mtu asiyekuwa na shukrani na mema aliyoifanyiwa na serikali yake...

Alhabdulillah nimepata kaesposure uchwara na baadaye nakuja kugundua upinzani ni kitu tofauti, kwanza nachukizwa na matumizi ya neno mpinzani kwa maana ya tafsiri ya mtu anayetaka haki na usawa kwenye mambo muhimu na ya msingi kijamii...ni tusi kumwita mama yangu aliyeota malenge lenge mikononi kwa sababu ya kuchakazwa na jembe la mkono wakati akiikataa serikali ya CCM inayohubiri kilimo ni uti wa mgongo wa taifa huku hawajui kamusi zao kisiasa zikishindwa kumtambua mkulima ni nani!

Kwanini nisijiundie ibara yangu binafsi ya sheria na kumdefine rasmi mpinzani kama mtu anayeenda kinyume na matakwa ya msingi ya binadamu ambayo kwayo ndiyo njia aliyowarubuni nayo wananchi kwa slogan tofauti kuwakalia kimabavu?

Muda si mrefu watu watakuwa wamepata elimu ya uraia na watakuwa wanajitambua,na ndipo serikali ya CCM itang'olewa kama jino bovu. Binafsi siamini neno linaloitwa giza,huwa naita kukosekana kwa mwanga kwa muda na yeyote anayesema 'siwezi' abadili kauli aseme nimekosa namna ya kupata suluhisho!
 
Kuitetea ccm mpaka unywe viroba kwa akili ya kawaida huwezi chama kishaoza
 
Hao ni sikio la kufa mtu , wote waroho wa madaraka na rasilimali za nchi hii.
 
Jamani eee , mbona viongozi wetu walikuwa huko juzi tu na wakaibuka na hii mizigo ? Mnataka nini tena ?
 
Rio Ferdinand = Mwigulu
Nemanja Vidic = Nape

Unategemea nini hapo? Uchochoro huo!
 
UKiona hoja zinajibiwa matusi matusi inamaanisha uwezo wa kufikiri kwishiney haijalishi mtoa hoja ni chadema au ccm
 
Back
Top Bottom