VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Sasa ni dhahiri kuwa CCM inazidiwa ujanja wa kisiasa na CHADEMA na wengineo. Wakati CHADEMA,wapinzani wetu wa jadi, wakichanja mbuga na kupasua anga kwa chopa kujenga chama chao,sisi CCM tunaketi maofisini na kupiga majungu na kujadili makundi/kambi ndani ya chama. Sasa tunaelekea pabaya. Kama chama tawala,inabidi tujipange upya kupambana kisiasa.
Kutwa kucha kushinda Lumumba, Makao Makuu Dodoma na Ofisi nyinginezo kupanga makundi ndani ya chama na kuchagua pa kuibuka napo 2015.Basi. Kweli!? Kwani viongozi wa 2015 tutachagua sisi CCM peke yetu? Si wananchi wote wa Tanzania wenye umri na sifa nyinginezo za kupiga kura? Hatufanyi haki kwa chama chetu. Tunakiangamiza.
Umefika wakati wa mabadiliko. Matamko ya Katibu wa Itikadi na Uenezi hayatakibeba chama. Nasi twende kwa wanachi.Wao pale;sisi kule. Tusibaki maofisini na kuishia kupendekeza kufukuzana kwa wale wanaothubutu kuendana na moto wa demokrasia yasasa ya nchi. Mambo yamebadilika. Siasa imeimarika. Majungu,fitina,makundi,kubweteka na kujiamini ndio maadui wakuu wa kukiangamiza chama chetu cha CCM.
Tubadilike.Tuwajibike.Tusonge mbele.Kwa hali ilivyo sasa (kwakuwa nimetembelea mikoa mbalimbali na kushuhudia shughuli za chama), CCM beki hazikabi.Watendaji badala ya kutegemea hoja zao na yale yaliyotekelezwa Kiilani,wao wanategemea vyombo vya dola. Hii haisaidii. Tunapotea. Hata kama hatuna chopa,twende hata na magari. Muda ni huu.
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam