CCM: Bajeti ikapite

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Umesambazwa ujumbe kwa njia ya simu na imeili kwa kila Waziri atokaye kila mkoa wa Tanzania ili awafikishie Wabunge wa CCM wa mkoa wake kuwa Bajeti ya Serikali ikapite bila bughudha yoyote. Kila Waziri au Naibu Waziri wa mkoa husika ameamriwa na Kamati Kuu ya CCM kuongea na Wabunge wa Mkoa wake na kuwaagiza kuwa wote wanaiunga mkono Bajeti kuu pamoja na za kila Wizara ya mwaka huu. 'Wabunge wote wa CCM kuanzia tarehe 9/4/2013 wawe kitu kimoja. Asitokee Mbunge wa kusababisha kuitishwa kwa caucus(kikao cha Wabunge wa chama). Huyo ashughulikiwe haraka. Sasa tutakuwa macho.Hii ni amri.' ulionya ujumbe huo ambao umeelekezwa kwa Mawaziri toka Kamati Kuu ya CCM. Je, tutafika kwa udhibiti huu wa fikra? VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam.
 
Last edited by a moderator:
Hata kwenye uchaguzi mkuu watatuma sms kwa kila mwananchi aichague au?
 
Najua kabisa safari hii kutachimbika bungeni, pamoja na udogo wa wabunge wa upinzani lakini wataonyesha kuwa wanaweza.
 
Kwa hili wabunge wa ccm hawathubutu tena kuitisha hata mkutano majimboni kwani wananchi wamewashtukia kuwa wanapalilia kibarua chao chamani.ndo maana magamba wamechokwa
 
Hata kwenye uchaguzi mkuu watatuma sms kwa kila mwananchi aichague au?
Mbona 2010 ndiyo walifanya hivyo? Tena zilitumwa sms zenye utambulisho wa Jakaya Kikwete. Watu wa bush wasiojua hili wala lile walipoona message ya Kikwete wakawehuka eti hadi mimi nimetumiwa ujumbe na Kikwete? Na wakatumia mbinu hiyhiyo pia kusambaza udini. Kwani CCM wanajali? Wao wanachokiwaza ni kuendelea kuongoza tu, it doesn't matter how they get there!
 
mbona sijawahi kufikiria juu ya kukwama kwa bajeti chini ya bunge la wasinziaji wa ccm.
 
Hii inajulikana wazi tegemeo la wananchi limebaki kwa wabunge wa CDM na baadhi ya wapinzani, waacheni waendelee kujichimbia mashimo 2015 siyo mbali, mradi wananchi waachiwe kuona Bunge live ili mwisho wa siku watoe hukumu wenyewe.
 
Kama wameandaa bajeti nzuri kwanini ipite kwa biti?
 
Mkakati wa kuwafungia wabunge wote machachali wa cdm ili bajeti ipite bila purukushani si mnauona?:shut-mouth:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…