VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Nasajili ukweli wangu leo. Nimekuwa chamani, CCM kwa miongo kadhaa. Nimewajua watu,vitu na sehemu mbalimbali. Presidential material si mtu mmoja. Ni mfumo ambao ndio utakaochukua hatamu. Kama ulivyo Urais wenyewe ulivyo si binafsi,mgombea si binafsi. Ndani ya CCM kwasasa hakuna.
Mfumo huwa na malengo yafananayo. Ndani ya CCM,kila mtajwa kawa mgombea mtarajiwa ana wafuasi maslahi tu wenye maslahi tofauti. Wanapelekeshwa na haja zao na si hoja zao. Mawazo na malengo tofauti hayajengi mfumo. Kukosekana mfumo thabiti ni kukosekana presidential material.
Nasema,bado hakuna mwenye mfumo wa kuwa Rais ndani ya CCM na hivyo mwenye sifa hayupo. Vyombo vya habari vitatumika kupamba na kuremba. Lakini,hakuna mwenye sifa. Pesa na hisa vitatumika kisiasa na kwa mikasa.Watanzania watalishwa kasa wasipokuwa makini.
Mzee Tupatupa wa Lumumba (sasa Ruvuma)