CCM Babati Washikana Uchawi

Zapa RadioFm

Senior Member
Feb 12, 2016
112
171
Babati. Viongozi watatu wa CCM waliofukuzwa uanachama, wamedai kuwa hawatambui hatua hiyo iliyofanywa na Halmashauri ya Mkoa wa Manyara.

Wakizungumza leo kwa nyakati tofauti, viongozi hao wamedai kuwa kabla ya hapo hawakuwahi kupewa onyo kwa njia ya barua au mdomo, hivyo hawatambui kufukuzwa kwao.

Cosmas Masauda amesema bado ni mjumbe halali wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa akiwakilisha Babati Mjini na ameshaandika barua ngazi za juu za chama hicho ili kupinga kufukuzwa kwake.

“Niligombea ubunge kwenye kura za maoni mwaka 2015 nikiwa na wenzangu wanane, ila kura hazikutosha. Kitu kilichosababisha CCM ishindwe Babati ni kusimamisha watu wasiokubalika kwa wananchi,” amesema Masauda.

Mjumbe mwingine wa mkutano mkuu wa chama hicho ngazi ya Taifa, Zulekha Mohamed alisema anatambua nafasi zake mbili kwenye chama hicho kwa kuwa hakuwahi kuitwa sehemu yoyote kuambiwa kosa lake. “Zaidi ya wadhifa huo, pia mimi bado ni mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Babati Mjini, hivyo sitambui kufukuzwa kwangu na nimeshaandika barua ya kupinga,” amesema Mohamed.

Amesema mwaka 2015 aligombea udiwani viti maalumu Babati Mjini, hivyo asingewaombea kura wapinzani kwa kuwa ushindi ulitakiwa kwa chama chao.

Katibu wa CCM Mkoa wa Manyara, Ndengaso Ndekubali alisema waliofukuzwa wazingatie katiba na kanuni na kama wanaona wameonewa na kikao cha halmashauri ya mkoa wakate rufaa ngazi za juu.

Februari 25, mwaka huu, Halmashauri ya CCM mkoani Manyara iliwafuta uanachama Masauda, Mohamed na Mjumbe wa Kamati ya Maadili wa mkoa, Felix Kivuyo na kuwavua nyadhifa viongozi 18 wa Kata za Babati na Mbulu.
 
Wakomae. Baada ya CCM kumbeba Chambiri,aliyekamatwa kwa rushwa na ambaye aliunderdeliver ndio sababu ya kupigwa chini ukiachilia nguvu za Gekul Pauline
 
Back
Top Bottom