CCM Arusha bado kwafukuta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Arusha bado kwafukuta

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Jan 17, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Ajenda za kutaka kung’olewa kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda, na baadhi ya wajumbe kupinga hatua iliyochukuliwa katika kikao kilichopita cha Halmashauri Kuu ya CCM mkoani hapa cha kuwapa onyo kali baadhi ya

  wananchama na wengine kusamehewa, kumetajwa kuwa sababu ya kuvunjia bila kufikia muafaka kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa kilichofanyika juzi jioni.

  Hoja ya kupinga kupewa onyo kali huku wanachama wengine wakisamehewa licha ya makosa yao kuwa sawa, inawahusisha

  baadhi ya wanachama wa Umoja wa Vijana CCM walioshiriki maandamano ya kumpinga Chatanda katika uzinduzi wa mashina ya umoja huo hapo mwaka jana ambapo wanadaiwa kuwa walifanya bila kufuata taratibu za chama.

  Ilielezwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (CC), Stephen Wassira, alipotembelea mkoani hapa, alikutana na uongozi wa

  CCM mkoa ambapo pamoja na mambo waliyoyazungumza kikao hicho kilichukua uamuzi wa kuwasamehe na wengine kupewa onyo kali.


  Katika kikao cha juzi, hali ya kutoelewana ilianza baada ya kupata taarifa ya maamuzi ya kikao kilichopita na kuwafanya wengine watake kuingizwa kwa hoja ya kung’olewa kwa Chatanda kwenye wadhifa wake.

  Inadaiwa kuwa Mwenyekiti wa kikao hicho, Onesmo Nangole, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa, aliwataka wajumbe

  kupiga kura za kutokuwa na imani na Chatanda, kutokana na kukidhoofisha chama, hatua ambayo iligomewa na wajumbe wengine.


  Habari zilisema hoja ya kutokuwa na imani na Chatanda iliungwa mkono na mjumbe mmoja kutoka Longido na kuwafanya baadhi ya wajumbe kuona kuwa taratibu zinazotumika kuingiza ajenda katika kikao hazikuwa sahihi kwani utaratibu unaotumika ni kamati ya siasa ya mkoa ndiyo inayoingiza ajenda za mkutano.


  Mzozo huo ulimfanya Nangole kuahirisha kikao na kuamuru Kamati ya Utekelezaji na Kamati ya Siasa kurudia upya maazimio ya kikao kilichopita ili yawasilishwe upya katika kikao kijacho cha mkoa.

  Alipozungumza na waanahabari kuhusu kikao hicho, Chatanda alidai kuwa kikao hakikuvunjika na kwamba ajenda ya kung’olewa wadhifa wake haikuwepo.

  Hata hivyo, alisema uamuzi wa kuwapa adhabu vijana waliofanya maandamano ya kumpinga na wengine kusamehewa yalitolewa na kikao cha Kamati ya Siasa ya Mkoa.

  Alisema yeye alikubaliana na maamuzi hayo na akataka adhabu kali zaidi zichukuliwe dhidi ya wahusika.

  Alisisitiza kuwa ajenda zote zilijadiliwa kama kawaida ingawa, lakini habari zinadai kuwa kikao hicho kilichoanza saa 3:00 asubuhi na kuendelea hadi saa 12:00 jioni bila kufikia muafaka kilikuwa na ajenda saba.


  CHANZO: NIPASHE

   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Jan 17, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Hivi CCM bado wapogi Arusha?
  Mbona hawana chao hapa si watakuwa wanapoteza muda tu?
  CCM hapa Arusha tulishakizika zamaniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!!!!!!!!!!!!!!
   
 3. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mi naona wanakujaga kuchukua kodi ya lile jengo lao tu!

  Mafisadi mbinu zao tunao mfukoni!

  Kwisha hbr yao!
   
Loading...