CCM Ardhini vs UKAWA Angani

CCM Ardhini vs UKAWA Angani

Mr Chin

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
4,625
Reaction score
1,024
[h=3]LOWASSA ANGANI VS MAGUFULI ARDHINI[/h]

11986557_960445247332227_8370133530535306079_n.jpg

Wakati mgombea urais wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, ameanza harakati za kuomba kura kwa wananchi kwa kutumia helkopta (Chopa) baada ya kuchoka na kudhoofika kwa kutumia usafiri wa ardhini, mgombea wa nafasi hiyo kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, ataanza kuuteka Mkoa wa Morogoro leo kwa staili ile ile ya kutumia Magari.

Lowassa ambaye ameanza kampeni mikoani Jumamosi iliyopita alikuwa akitumia usafiri wa magari, huku kwa siku alifanya kati ya mikutano miwili hadi mitatu. Mikoa ambayo hadi jana mgombea huyo na msafara wake walikuwa wamefanya mikutano ya kampeni ni Iringa, Njombe, Rukwa na Katavi. Leo Lowassa yupo mkoani Kigoma ambapo atakuwa anatumia usafiri wa Helkopta.

MAGUFULI ARDHINI Baada ya siku kumi za milima, mabonde, barabara za lami, vumbi, njaa, jua, manyunyu ya mvua, za kutembea takribani kilomita 4,000 kutoka Dar es Salaam hadi Katavi na kuelekea Mtwara kukamilisha ngwe ya kwanza, mgombe wa urais wa CCM, Dk. Magufuli, amefanya takribani mikutano 80. Zilikuwa siku za kupata ajali ndogo, magurudumu kupungua upepo na baadhi ya magari kubaki nyuma, wakati mwingine kupotea njia baada ya kuachwa. Kazi hiyo leo imehamia mkoani Morogoro kwa mgombea huyo kutafuta ridhaa ya wananchi kumpigia kura za kutosha zitakazomwezesha kuingia Ikulu Oktoba 25, mwaka huu.

Mh. Magufuli anaonyesha uimara wa kuwa Head of State kwa kwenda kila Kata, Jimbo, Wilaya na Mkoa kwa kutumia usarifi wa ardhi. Huyu ndie Mgombea anaye weza kuiongoza Tanzania. Mungu Mbariki Mh. John P. J. Magufuli.
 
Mimi hata sijakuelewa kabisa. Ukiweka jiwe na Magufuli/CCM, nitachagua jiwe.

Twende na Lowassa/UKAWA
 
Miaka zaidi ya 50 hakustahili kupita kwenye barabara na magurudumu kuisha upepo, kupata ajali na kupotea njia. Hii inaonyesha serikali ya chama tawala imechoka mpaka mgombea wake anapita maeneo yasiyo salama. Tusijisifie kwa umaskini.
 
It happened to Obama as well, you must be living in Utopia land.
 
Mimi hata sijakuelewa kabisa. Ukiweka jiwe na Magufuli/CCM, nitachagua jiwe.

Twende na Lowassa/UKAWA
Kwasabau akili yako ni jiwe ndio maana huna uwezo wa kufikia zaidi ya ujiwe jiwe tu.
 
Magufuli ana tumia gari ili azifahamu shida za wananchi ambazo alikuwa hazifahamu kwa kuwa alikuwa hana haja nao.

Lowassa ana tumia helkopta ili imuwaishe kwenda kupanga mipango ya kutatua matatizo ya wananchi kwa kuwa ana zifahamu kwa kuwa ni mtoto wa masikini.
 
Uhaifu ndio umemkimbiza jamaa yenu . Hana uwezo wa kupigana vita ya ardhini. Watu wapo ardhini, mitaa ipo ardhini, na sio angani.
 
kumbe Magufuli kupita barabara zenye vumbi nayo ufahari?? Jamani tuangalie na mambo ya kujivunia. hii thread ni kichekesho
 
ccm wamewatesa na kuwadanganya watz kwa muda mrefu mno ngoja warambe vumbi na wasubr kichapo hapo oct 25 .

unafiki
uzandiki
ufisadi
ulaghai
wizi
matusi
ubabaishaji
vitakuwa ni mwisho wenu
 
Mkuu angeonyesha uimara zaidi na kupata sifa nyingi kama angetumia usafiri wa baiskeli au angetembea kwa miguu kabisa !
 
iandaliwe chopa hata tatu,watumie akina samia,mwigulu,makongolo,kisha yeye aendelee kuchanja mbuga,ili kuondoa nyodo za timu lowasa kuwa wanatawala anga,si mnawajua hawa jamaa kwa majisifu
 
Back
Top Bottom