CCM acheni ushamba!

CCM acheni ushamba!

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
5,255
Reaction score
8,027
Mahakama ya juu nchini Kenya haikumpa ushindi wa Urais Raila Odinga,haimaanishi kua uchaguzi ukirudiwa ndio Odinga atashinda, imeamuru uchaguzi urudiwe.
Uhuru Kenyatta na Jubilee yake ndio wenye wabunge wengi bungeni kwahiyo bado safari ni ndefu.

Hii ni dhahiri kabisa kua wanaofikiria mbele zaidi ndani ya CCM hakuna.Wakati mnashangilia ya Kenya hamuoni kabisa kua huku wetu mahakama hairuhusu matokeo ya Urais kurudiwa? Hamuoni kua hiyo haki walioipata wenzetu wa NASA huko Kenya huku kwetu Tanzania hakuna?

Hamuoni kabisa hili linawatia moyo mahakimu na maji wetu kuacha kupokea maagizo yenu kufanya maamuzi zaidi na watafuta sheria? Hamuoni kua hili linawaamsha wapinzani kuidai katiba bora? Hamuoni kua Mahakama ikitenda haki CCM hamtasasilia kabisa?

Badilikeni bhana, acheni ushamba huo. Mnatakiwa mjifunze na sio kushangilia. Hili lina faida kubwa sana kwa wapinzani zaidi kuliko kwenu ninyi.
 
Washamba alafu wanaongozwa na wakuja
 
Bado Uhuru ana nafasi kubwa sana, hasa baada ya Raila kujinasibu atakuja na sera za raisi wetu. Wenzetu ni mabepari, hawapendi kusikia habari za kijamaa. Nakuahidi kuwa hutasikia Rais wetu akitajwa nngwe hii. Raila keshasomeshwa!
 
Ninyi ndiyo hasa mlisababisha 'mtaguro' huu! mbona mnahamaki!
 
Back
Top Bottom