CCM: Acheni kuiaibisha Serikali awamu ua nne

CCM: Acheni kuiaibisha Serikali awamu ua nne

diunal

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2013
Posts
498
Reaction score
70
Nimekuwa nikifuatilia mikutano ya hadhara ya kampeni ya Chama Cha Mapinduzi iliyokwishafanyika, na hata inayoendelea kufanyika.

Kuna mambo kadhaa ambayo CCM huenda mnajichanganya wenyewe kwa Serikali mnayoisimamia ninyi.
1. Tuhuma za Ufisadi Richmond dhidi ya Bwana Edward Lowassa imekuwa ni wimbo wa kila siku na usio na tija tena katika Kampeni za CCM. SWALI, kama huyo Mgombewa wa UKAWA alishiriki kuiba fedha za Watanzania, kwanini asichukuliwe hatua za kisheria kama ilivyo kwa akina Mramba na Yonah? Kwamba Serikali inamuogopa au Tatizo ni nini? Miaka 8 sasa imepita tangu ajiuzuru

2. Sheria ya nchi inasema kuwa endapo kuna mtu anayemiliki mali ambayo haielezeki katika uhalali wake ni sharti afunguliwe mashtaka. Sasa kama akina Yusuf Makamba wanadai Bw. Lowassa ana makandokando mengi tangu mwaka 1995, tuelewe au tutafsiri vipi juu ya uwezo wa serikali wanayoisimamia dhidi ya watu wa aina hiyo katika kuchukua hatua za kisheria?

Wito wangu kwa makada wa CCM mnaotoa kashfa kwa watu fulani mnapokuwa katika majukwaa ya mikutano ya hadhara hali mkiivua nguo Serikali yenu sio suala jema.

Ushabiki bila hekima ni kujiaibisha.
 
Nimekuwa nikifuatilia mikutano ya hadhara ya kampeni ya Chama Cha Mapinduzi iliyokwishafanyika, na hata inayoendelea kufanyika.
Kuna mambo kadhaa ambayo CCM huenda mnajichanganya wenyewe kwa serikali mnayoisimamia ninyi.
1. Tuhuma za Ufisadi Richmond dhidi ya Bwana Edward Lowassa imekuwa ni wimbo wa kila siku na usio na tija tena ktk Kampeni za CCM. SWALI, kama huyo Mgombewa wa UKAWA alishiriki kuiba fedha za Watanzania, kwanini asichukuliwe hatua za kisheria kama ilivyo kwa akina Mramba na Yonah? Kwamba Serikali inamuogopa au Tatizo ni nini? Miaka 8 sasa imepita tangu ajiuzuru
2. Sheria ya nchi inasema kuwa endapo kuna mtu anayemiliki mali ambayo haielezeki katika uhalali wake ni sherti afunguliwe mashtaka. Sasa kama akina Yusuf Makamba wanadai Bw. Lowassa ana makandokando mengi tangu mwaka 1995, tuelewe au tutafsiri vipi juu ya uwezo wa serikali wanayoisimamia dhidi ya watu wa aina hiyo katika kuchukua hatua za kisheria?

Wito wangu kwa makada wa CCM mnaotoa kashfa kwa watu fulani mnapokuwa katika majukwaa ya mikutano ya hadhara hali mkiivua nguo serikali yenu sio suala jema. Ushabiki bila hekima ni kujiaibisha.

Kwani wao ccm watakuelewa?!. Wao ni ushabiki kwa kwenda mbele
 
Umenena jambo la mbolea mkuu wanakiabisha chama chao kwa Ushabiki USO na mashiko
 
Laiti wananchi wangekuwa wanaruhusiwa kuwahoji baada ya maelezo yao, nadhan wasingerudia tena hizo sera. Hata hivyo ujumbe ushawafikia
 
Back
Top Bottom