CCK: Manumba amelidhalilisha Jeshi la Polisi

Kalunguine

JF-Expert Member
Jul 27, 2010
2,543
134
*Wamtaka awajibike kwa kukanusha madai ya Dkt. Mwakyembe
Na Reuben Kagaruki

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Kijamii (CCK), Bw. Lenatus Mwabi, amesema kitendo cha Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Bw. Robert Manumba kudai kuwa ugonjwa ambao unamsumbua Naibu Waziri wa Ujenzi Dkt. Harrison Mwakyembe hautokani na kulishwa sumu, kimelidhalilisha Jeshi la Polisi.

Akizungumza na Majira Dar es Salaam jana, Bw. Mwabi alisema kitendo cha Bw. Manumba kukanusha madai hayo katika vyombo vya habari, kinadhihilisha kuwa utendaji kazi wake umelenga kulinda maslahi ya watu wachache badala ya Watanzania wote.

“Kimsingi DCI Manumba amelidhalilisha Jeshi la Polisi, yeye mwenyewe na watendaji wa Serikali, taarifa aliyotoa kukanusha madai ya Dkt. Mwakyembe kulishwa sumu, inaonesha yupo kwa maslahi ya watu wachache si vinginevyo,” alima Bw. Mwabi.

Alisema kutokana na hali hiyo, alimtaka Bw. Manumba awajibike kwa kutekeleza majukumu aliyonayo kisheria kwani jukumu alilonazo ni kufanya uchunguzi ili kuwabaini watu ambao wanatuhumiwa kumpa sumu.

“Ukweli ni kwamba, kuna kitu kimeathiri afya ya Dkt. Mwakyembe, iweje atoke mtu nje ya maadili hadi Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda amshangae, kupewa sumu zi lazima mtu anyweshwe, alichokifanya Bw. Manumba, amemdhalilisha mgongwa anayedai kulishwa sumu.

“Ni kawaida ya Jeshi la Polisi kufanyia uchunguzi malalamiko mbalimbali ya wananchi, kwa mfano, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willbroad Slaa, aliwahi kutoa taarifa ya kuwekewa vinasa sauti katika chaga za kitanda kwenye hoteli aliyofikia mjini Dodoma lakini polisi hawakufanyia kazi,” alisema.

Alisema Dkt. Mwakyembe analilalamikia Jeshi la Polisi kwa kushindwa kufanyia kazi taarifa za vitisho alivyokuwa akipata kwa kuandika barua ya siri ambayo iliishia kuchapishwa katika vyombo vya habari.

“Hii inaonesha kuwa, jeshi letu halipo kwa maslahi ya Watanzania, hivyo Bw. Manumba anapaswa kuwajibike ambapo Mkuu wa Jeshi hili IGP Mwema, apime mwenyewe.

“Bw. Manumba amewakosea Watanzania kwa kushindwa kufanya kazi yake ipasavyo kwani hana mamlaka ya kuzungumzia suala zito linalohusu madai ya Dkt. Mwakyembe na kama atashindwa kuwajibika, wananchi wanaweza kuchukua hatua,” alisema.

Akizungumzia waraka unaodaiwa kusambazwa na Dkt. Mwakyembe kwa ndugu na jamaa zake wa karibu kuhusu chanzo cha ugonjwa wake, Bw. Mwabi alisema ni jambo zuri na ametumia njia sahihi.

Akizunguzia kauli zinazotolewa mara kwa mara na Waziri wa Afrika Mashariki, Bw. Samuel Sitta, kuwa Dkt. Mwakyembe amelishwa sumu, Bw. Mwabi, alisema Jeshi la Polisi linapaswa kuwa karibu naye ili aweze kuwapata taarifa za kina badala ya kutishia kumchukulia hatua za kisheria.


Hivi karibuni, Bw. Manumba alisema kitendo cha Bw. Mwakyembe kubeza utendaji kazi wa jeshi hilo baada ya kutoa taarifa za kukanusha kuwa ugonjwa unaomsumbua hautokani na kulishwa sumu ni mawazo yake binafsi.

“Mimi siwezi kuendeleza malumbano lakini fahamu kuwa, alichosema Dkt. Mwakyembe ni mawazo yake binafsi, hata wewe mwandishi unaweza kuzungumza chochote,” alisema Bw. Manumba.

Alisisitiza kuwa, majibu kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii yanaonesha kuwa, ugonjwa wa Dkt. Mwakyembe, hauhusiani na kulishwa sumu.

Akizungumzia madai ya Dkt. Mwakyembe kuwa alipeleka taarifa polisi za kutishiwa maisha yake Bw. Manumba alikiri jeshi hilo kupokea taarifa hizo na kuzifanyia kazi bila kufafanua zaidi matokeo ya uchunguzi huo.

source: gazeti la majira
 
Hii movie haina mwisho wakuu? Dr Mwakyembe aje atumalzie kwa kutaja hao wahusika mambo yaishe.
 
mambo ya nyumba ndogo haya hadi kupewa sumu then unatupotezea dira na mwelekeo tujadili kulishwa sumu na nyumba ndogo
 
mambo ya nyumba ndogo haya hadi kupewa sumu then unatupotezea dira na mwelekeo tujadili kulishwa sumu na nyumba ndogo

aku! kwa iyo unataka kunambia kuwa slaa aliwekewa vinasa sauti pale dodoma na nyumba ndogo??
 
aku! kwa iyo unataka kunambia kuwa slaa aliwekewa vinasa sauti pale dodoma na nyumba ndogo??

Kma cck siasa zenu ndio hizi hamtafika mbali. sasa Slaa kaingiaje hapo? wewe ullishindwaje kujibu swali bila kumtaja Slaa?
mama chama chenu kinakalia msumari wa moto
 
Hiki chama cha Kijamii(CCK) hakitafika popote katika siasa za Tanzania..Chenyewe kinaangalia current issues na kukutana na wanahabari..yaani ni kama kudandia basi kwa mbele ili kifike upesi kwenye umaarufu.

CCK inatakiwa iibue issue na si kudandia issue(kama CUF).Ukiangalia sasa Dr.Slaa hapo anaingiaje kwenye issue ya Dr.Mwakyembe na Manumba?? CCK imefulia
 
Hiki chama cha Kijamii(CCK) hakitafika popote katika siasa za Tanzania..Chenyewe kinaangalia current issues na kukutana na wanahabari..yaani ni kama kudandia basi kwa mbele ili kifike upesi kwenye umaarufu.

CCK inatakiwa iibue issue na si kudandia issue(kama CUF).Ukiangalia sasa Dr.Slaa hapo anaingiaje kwenye issue ya Dr.Mwakyembe na Manumba?? CCK imefulia


tatizo lenu magwanda,mnapenda kutukana wengine wakati nyie hamtaki kuguswa,kuweni wastaarabu,kwani wakati mnasema habari za mwakyembe kulishwa sumu na nyumba ndogo na slaa aliwahi kuwekewa kinasa sauti katika mazingira ya kutatanisha,fikirini
 
Back
Top Bottom