CASH vs CASHLESS

Zerock

Senior Member
Joined
Sep 3, 2026
Posts
191
Reaction score
320
Toka naanza kutumia pesa zangu binafsi zimekuwa nikituma sana CASHLESS (VISA CARD), nikiwa na pesa cash ujue ni kwaajili ya tips na vitu vidogo ambavyo siyo vya bei kubwa (maji, snacks,soda n.k).

Nilipata shida kuzowea nilipoingia kwenye mazingira ya kutumia cash (Tanzania).

Mifumo ya Cash kwenye hii kasi ya teknolojia duniani ni uzembe wa hali ya juu,
Imagine hadi leo hii watu wanatembea na furushi la pesa kisa tu wanaenda kununua matumiz ya nyumban ya shiling 20.
Kwanini kila duka lisiwe na lipa namba? Wenye maduka makubwa kwanini wasiwe na mashine za VISA?

Watu wengi wanapoteza/kuibiwa pesa Cash kwa kwa sababu hawana pa kuzitunza, au wanapo ila wanaogopa makato/tozo wakati wa kuzitoa.

Kuna ulazima wa kuhamisha akili zetu kutoka analogy kwenda digital.
 
Kwanini kila duka lisiwe na lipa namba? Wenye maduka makubwa kwanini wasiwe na mashine za VISA?
Nadhani kuna ultimatum kwa wafa ya biashara kupokea cash.

Kuna nchi ukiwa unataka kulipa cash unapangishwa foleni ndefu kuku discourage.
 
TIPS tanzania wanakata pesa nyingi sana kama service fees. Inakatisha Tamaa sana, ila wafanya biashara wengi wameendelea unakuta mpaka stationery ina lipa No. mpaka Genge la mama ntilie liko na lipa no. ila kwakua makato anakatwa mteja basi watumiaji ni wachache
 
Elimu ndogo pia makato makubwa sana. Mwenye nafuu ni azam pesa tu. Kwanza nenda kakkoo weng unakuta anakwamnia lipa namba ina shida ndio mpaka unashangaa shida gam kumbe aanahis atafatiliwa kodi kule. Unakuta mitandao wana lipa namba zao ila makato yake makubwa utafikir wanahamisha pesa. Teeego ndio balaa
 
Cashless huku kwetu ni "An expensive convenience "! Nakuapia utafilisika. Sio kwa tozo hizo!
 
Cashless huku kwetu ni "An expensive convenience "! Nakuapia utafilisika. Sio kwa tozo hizo!
Hiyo ndo changamoto iliyopo,inakatisha tamaa, ndio maana watu wanaamua kutembea na furushi la pesa cash
 
Serikali imekuja kuongeza ugumu wa watu kuhamia kwenye cashless,kila sehem foleni ya tozo na ushuru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…