Carl Max na falsafa ya matabaka

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,743
25,535
SOMA KWA AJILI MAARIFA YAKO NA VIZAZI VYAKO
1.TABAKA LA JUU.
2. TABAKA LA KATI
3. TABAKA LA CHINI.
Kwa mujibu wa mwanafasafa Carl Marx, katika maandiko yake yeye na mwenzake Friederick Engel, wanaamini kuwa tabaka la kati ndio lenye uwezo wa kufanya mapinduzi ya ndani, wakati yanapohitajika.
Tabaka la kati, linaundwa hasa na watu wa kipato cha kati ambao wengi wao ni watumishi wa umma; wataalamu wa afya, walimu, wakandarasi, wanasheria, wafanya biashara wa kati, askari, waandishi nk.
Kundi hili linapoamua kuwa mashabiki wa kundi la watawala, ambao wengi wao wanaishi maisha ya ukwasi mkubwa, maisha ya paradiso, basi kundi lile la tatu yaani watu wa kipato cha chini wanabaki yatima bila watetezi.
Waandishi wasipoandika upuuzi wa watawala, wanasheria wasipokemea upuuzi wa watawala, madkatari, walimu na wakandarasi wasiposema mapungufu ya watawala katika kuboresha huduma mahali husika, wakaamua kuwa wapambe wa serikali, wakaamua kuwa wapiga debe, wapiga ngoma, wapiga filimbi, wakereketwa wa watawala, basi watawala wataendelea kuishi maisha ya mbinguni huku watu wa kipato cha chini, masikini wanaokula minyoo, wanaoishi na kunguni na panya ndani ya malango yao, hawatakuwa na mtetezi. Nao watadumu katika maisha hayo ya afadhali ya jana hadi mwisho wa dahari.
Lakini endapo tabaka la kati, litakataa kuwa vibaraka wa serikali na kufanya kuikemea, kuielekeza, kuikosoa, kuikumbusha, kuiangaliza, kuishauri na kuibeza; hapo ndipo serikali itachangamka kwa kuwa kundi hilo lina nguvu kubwa. Ndio kundi linalozalisha na kulipa kodi.
Lakini Carl Marx anaonya kwamba, endapo watu wa tabaka la kati wataacha kuwa wapambe wa serikali, wakaanza kunipinga kwa maovu yake, na ikiwa serikali ni kichwa ngumu basi hapo ni sawa na ku'commit suicide', ni sawa na kujitoa uhai. Serikali dhalimu inayoongozwa na majuha haitaki kukosolewa, kushauriwa, kubezwa, kuangalizwa, kukumbushwa nk. Haitaki fasihi. Na yanapotokea hayo wasioyataka, basi ardhi hupata kunywa damu hadi pomoni. Kucha na meno kung'olewa kwa koleo tena bila ganzi. Kumbe haitoshi tu kwa tabaka la kati kuwa na nguvu ya kuichangamsha serikali bali pia ili nguvu hiyo ionekane ni lazima kufuta mstari unaotenganisha kifo na uhai. Katikati ya serikali katili, lazima kujiitoa. Ni kazi ambayo mabwege hawawezi kuthubutu.
Muungano wa kisoviet, chini ya Vladimir Lennin, ulifanikiwa kwa kuunganisha wafanyakazi ambao ni tabaka la kati, chini ya kauli mbiu "ALL WORKERS UNITE". Kama kuna mtu anatafuta silaha ya kuangamiza udhalimu katika taifa lake, silaha ya kwanza ni kuinganisha vyama vya wafanyakazi. Fikiria, madaktari, walimu, wanasheria, wanafunzi wa vyuo vikuu, wakandarasi, waandishi na wataalamu wengine wakakubaliana pamoja! Kwa maslahi ya umma! Fikiria tu.

Mungu Ibarik Tanzania.
Mungu ibariki Afrika.
 
Mungu Ibarik Afrika
Mungu ibariki Tanzania

Kwa nini umeanza na Mungu Ibariki Afrika kwanza kabla ya Tanzania? Ni lazima Mungu aibariki Tanzania yetu kwanza halafu ndiyo Afrika!
 
Ikiwa karne hii umetuletea fikra hizo za Kikomunisti basi ipo haja ya kutolewa dira ya kifalsafa ya maisha ya Kitanzania. Toka Ujamaa wa Mwalimu inaonekana kuna ombwe fulani hivi. Mambo hayo yalikuwa ni lulu miaka ya 70. Mashuleni tulijifunza sana hayo. Ikiwa ni somo la siasa ama la uchumi hasa A Level. Pale kwenye V. I Ulyanov (Lenin) waunganishe "Bolsheviks", na kwa Usovieti mweke Joseph Stalin. Halafu kwenye kauli mbiu hiyo weka "The Communist Manifesto" ambayo kirefu cha hayo ulioandika kwa ufupi kilikuwa: "Workers of all lands unite. You have nothing to lose but your chains." Ila kuturudisha huko ni sawa sawa na kurudisha nyuma gurudumu la kimaendeleo la jamii ya mwanadamu na fikra zake.

Ukomunisti japo ulikuwa na falsafa nzuri kiasi fulani ulikiuka sana haki za kibinadamu. Ukomunisti ulimtenga Mungu mbali na maisha ya mwanadamu. Walihubiri udikteta wa wafanyakazi "Dictatorship of the Prolerariat." Walikataa Ubepari lakini dola ikageuka kuwa ya kibepari "State Capitalism." Kamati zilizosimamia mali ya umma ziligeuza mali ile kuwa ya kwao. Uhuru wa habari na kujieleza ulizimwa. Urusi ilikuwa na mbinu moja mbaya sana ya upotoshaji wa habari wenyewe waliita:"Disinfomatsiya." Inasemekana kwa miaka mingi sana Marekani walidhani Urusi ya Kisovieti ilikuwa na nguvu sana hadi pale ilipoanguka ndipo wakajua walihadaiwa kufikiri hivyo.

Ukomunisti uliwaogopa wasomi kama akina Aleksandr Solzenitsyn mwandishi wa 'The Gulag Archipelago," na vitabu vingine.Leon Trotsky (Mkomunisti wa mrengo wa kati) alipopingana na Stalin na kutorokea Mexico alifuatwa huko na kuuawa mwaka 1940 . Karl Marx mwenyewe anashutumiwa kwa kuitelekeza familia yake na kushindia London Library akisoma na kuandika. Kama si Friedrich Engels maisha yangemshinda.

Ukomunisti haufai leo. Hata Kiongozi mkuu wa Komsomol Umoja wa Vijana wa CPSU, Sergei Kourdakov, mwaka 1970 aliukimbia na kutorokea Canada na kuwa Mkristo baada ya kugundua upungufu wa Ukomunisti. Ulimwengu wa leo umestaarabika hatuhitaji tena fikra za Karl Marx na Lenin kivile. Wala hatuhitaji fikra za kimapinduzi za kumwaga damu ama kuleta fujo katika jamii. Hatuhitaji "Black September" wa kuteka ndege nyara ili kujieleza kero zao. Ukitaja majina ya akina George Habash, Leila Khaled ama Abu Jihad miongoni mwa vijana wa leo Ukanda wa Magharibi hata kusisimuka hawasisimuki. Hauwatambui kwa jinsi walivyojulikana miaka 40 iliyopita.

Ulimwengu umebadilika sana. Usiturudishe huko kwenye enzi hizo. Hatuhitaji migomo ya wanafunzi wa chuo kikuu kama vile ule wa Kent State University Mei 4, 1970 huko Marekani. Tuwaze mapya tutafute falsafa mpya ya kimaisha na kimaendeleo ya taifa letu. Tujenge uzalendo wa kweli. Tuipende nchi hii na mustakabali wake. Kama tuna misingi mizuri ya kifikra iliyowekwa hapa awali na wazee wetu basi tuichambue na tuipe sura ya kisasa itusaidie. Tutasonga mbele.
 
Back
Top Bottom