Ninamkumbuka John Komba miaka ya mwisho wa 70 na mapema 80 alikua mwalimu wa shule ya msingi Kana, Tanga mjini. Kipaji chake cha kuimba kiliipa shule ya Kana umaarufu wa hali ya juu kwenye kwaya. Nyimbo ninayokumbuka ni nchi yangu Tanzania. Maudhui yalikua; "nchi yenye watu wengi, siasa safi kwa wote na uongozi bora".