voicer
JF-Expert Member
- Jul 13, 2020
- 5,545
- 11,943
Naam!
Hamkani upepo si shwari ndani bahari ya Hindi. Nahodha mkuu wa Jahazi tulilopandia njiani kutokea mji wa 2020, amejaa jazba ghafla na jahazi linaendeshwa kwa hasira zaidi kuliko Busara.
Pia ni kama vile hamuamini Kapteni Mkuu kwenye hili jahazi letu kwenye dhoruba hii ya kuufikia nji wa 2025. Ulioko Pwani ya bahari ya Hindi.
Kasi ya Jahazi kuvuja inazidi kuwa kubwa. Matobo yanazidi kuongezeka huku kwa mbaali abiria wakianza kurudisha Tiketi za Chombo walichoko ndani yake.
Kapteni mkuu katelephone amewekewa kapteni msaidizi Be - take!
Ni dhahiri kwamba kuna Ufa au kuna shinikizo fulani aidha toka pembeni kwenye lile kundi la abiria wenye Mzigo mkubwa ndani ya Jahazi.
Ambao wanaona Kapteni mkuu anakuwa ni kikwazo kwao pale wanapotaka kupakia mizigo isiyoruhusiwa ndani ya Jahazi.
Ni dhahiri shayiri kwamba siku za U-kapteni mkuu Katelephone kuelekea 2025, zinazidi kuhesabika.
Ni suala la muda tu, kulingana na hasira kubwa na ghadhabu aliyonayo Bi Nahodha kwa sasa.
Nikushauri ewe Kapteni mkuu Katelephone na hasa sisi abiria wadogo wadogo
Tunayo Imani na wewe hivyo Anza kuishi na hao abiria wakubwa kwa akili kubwa.
Itakapofika wakati sahihi,
Vema ukaruka na kujitosa nchi kavu na utafute Nyumba nzuri ya kizalendo wewe na wazalendo wengine.
Mjitafute na kujitoa kifua mbele ndipo mtakapoona Abiria wote kwa asilimia kubwa wakinunua tiketi za kuingia kwenye Jahazi lenu ili kuliokoa Jahazi kuelekea mji wa 2025.