Tram Almasi
JF-Expert Member
- Feb 26, 2009
- 749
- 226
Mkuu, maandalizi na commitment hakuna miujiza hapo!
EMTKile kisiwa kidogo chenye watu laki tano tuu Cape Verde kimefanikiwa kuingia kwenye fainali za Kombe la Afrika (Africa Cup of Nations) baada ya kucharagaza Cameron na akina Eto'o. Cameroon wametupwa nje baada ya kufungwa jumla ya mabao 3-2 na haka kanchi. Cape Verde watacheza kwenye fainali mwakani South africa. Tanzania tuko wapi? Kanchi kama kama haka kanatinga finaili tena kwa kuichapa Cameroon, sie bado......
EMT
Umenifanya nicheke kidogo.
Hivi kuna vinchi vidogo duniani? Ina watu laki tano tu?
Hivi Cape Verde inaishi chini ya kivuli cha nchi ipi? Cape Verde inajitegemea? Je ni maskini kama Tanzania?
Nje ya mada kidogo...kuna mijadala hapa JF inasema Zanzibar haiwezi kuwa nchi.
Pili, Wapo wanaosema Zanzibar itaishi chini ya kivuli cha Tanganyika siku zote.
Je tumewazibia njia Zanzibar kuwa Cape Verde ya Tanzania?
Utaelewa kwa nini mada yako imenifanya nicheke kidogo.Jenerali Ulimwengu alishasema kuwa sisi Tanzania tumeamua kufanya "upuuzi" katika kila kitu. Baya zaidi ni kuwa hata huo upuuzi hatuupangilii. Hata kama tutafurahi kuwa mabingwa katika kufanya upuuzi basi hatutachukua nafasi ya kwanza kwani Congo/ Zaire ambayo inaongoza kwa upuuzi, yenyewe imepangilia upuuzi wake.
Link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...imwengu-hata-kwenye-upuuzi-tuko-dhaifu-3.html