Cameroon imemjibu Edo Kumwembe kwa kufuzu fainali

moesy

JF-Expert Member
Oct 30, 2012
3,555
3,535
Baada ya kuiponda Cameroon kwenye moja ya makala yake katika gazeti la MwanaSpoti, hatimaye timu ya taifa Cameroon( Simba wasiofugika) hapo jana wamemjibu Edo baada ya kumpiga Ghana 2 - 0.

Edo Kumwembe aliiponda sana Cameroon. Hii inatufundisha umuhimu wa kuweka akiba ya maneno.

========
Cameroon wataumana na Misri katika fainali ya kombe la mataifa ya Afrika 2017 baada ya magoli mawili ya kipindi cha pili kuiondosha Ghana katika mashindano hayo.

Timu zote mbili zilicheza mchezo wa kuvutia huku ikishuhudiwa kipindi cha kwanza zikimaliza kwa sare ya bila kufungana.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo milango ya kila timu iliendelea kuwa migumu mpaka dakika ya 72 Michael Ngadeu-Ngadjui alipofunga goli la kwanza kwa Cameroon.

Zikiwa zimesalia sekunde chache huku Ghana wakijaribu kusawazisha Christian Bassogog alifunga goli la pili na kuzamisha kabisa matumaini ya Ghana kwa mwaka huu.

Matumanini ya Ghana kuchukua kikombe hicho ambacho kwa mara ya mwisho walikibeba mwaka 1982 sasa yamefikia mwisho katika michuano ya mwaka huu.

Mara ya mwisho kwa Cameroon kuingia fainali ilikuwa mwaka 2008 walipofungwa na Misri ambao ndio wanakutana nao tena katika fainali ya mwaka huu.
 
Lupyeee,
Wewe ni goigoi hapa ni mada ya kimichezo wewe unachomekea siasa sijui kwa nini mods wanaendelea kuwaacha wapunbavu kama wewe kuendelea ku comment upumbavu Kama huu na mkaachwa kutamalaki come on mods make JF GREAT AGAIN!?
 
Hii thread ni ya habari ya michezo lakini vijana wa Lumumba na Ufipa wameigeuza uwanja wa vita....siasa na kubet ni vitu vinavyoua fikra za vijana bongo.
 
edo kumwembe hajacheza mpira proffessional... ila ujanja ujanja tu umempa uchambuzi...

unachambuaje kitu usichokijua..

dstv sio wajinga kuwaweka kina kuffor, ma carty, na wengineo x footballers
 
Back
Top Bottom