Sio kwamba sijui ile calculator kwenye mtandao wa TRA ila haifuatwi na tunabaki njia panda kujua ni kodi kiasi gani utatozwa iwapo uta import gari kutoka nje. Rafiki yangu ame import gari na akatumia TRA calculator kupata kiwango cha kodi na kaiandaa hiyo kodi ili gari likiwasili alipe bila usumbufu.
Cha kushangaza Gari lilipofika alienda kulipa ila akaambiwa kuna ongezeko la Tshs milioni 3. Hii inachanganya naomba TRA watueleze jinsi wanavyo calculate kodi ya car import na kama wameacha ile online calculator watuambie kwani ni kama wanatuvizia. Pia wanaweza kuingia kwenye mtandao mtu alikonunua gari na ku kadiria kodi ki uhakika kuliko kila mtu kukadiria anavyojua.